Friday, October 5, 2012

MARUKUFUKU DAMU KUUNZIWA WAGONJWA NCHINI






Wananchi Mkoani Tabora Wametakiwa Kuwafichua Watumishi Wa Afya Ambao Wanaowauzia.

Wagonjwa Damu Hospitalini Badala Ya Kutolewa Bure Ili Waweze Kuchukuliwa Hatua Za Kisheria Kwa Lengo La Kukomesha Tabia Hiyo.
 
Wito huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha  maabara katika benki ya Damu salama mkoa wa Tabora ,Thomas Njingo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana baada ya kutokea kwa wananchi kulalamika kuuziwa damu .
 
Alisema Wananchi Wakishikamana Pamoja Katika Kuwafichua Watumishi Wa Afya Wanaowauzia Wagonjwa Damu Inayotakiwa Kutolewa Bure Ni Dhahiri Kuwa Vitendo Hivyo Vitakomeshwa Na Wananchi Wataipata Huduma Hiyo Pasipo Usumbufu. 

Amefafanua Kuwa Kitendo Cha Wananchi Kuuziwa Damu Hospitalini Kinachangia Kwa Kiasi Kikubwa Watu Kukosa Imani Nao Hali Inayosababisha Washindwe Kuwa Na Mwamko Wa Kuchangia Damu Kwa Hiari Pindi Wanapotakiwa Kufanya Hivyo.

Njingo Amesema Damu Hiyo Ambayo Wananchi Huchangia Inapaswa Kutolewa Bure Kwa Wagonjwa Wakiwemo Wajawazito, Majeruhi Wa Ajali Mbalimbali Pamoja Na Watoto. 

Mkuu Huyo Wa kitengo cha  Maabara Amewasihi Wananchi Kutoa Taarifa Sehemu Husika Ikiwemo Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa- Takukuru Pindi Wanapoona Wagonjwa Wao Wanauziwa Damu Inayopaswa Kutolewa Bure Na Kwamba Hawatasita Kuwachukulia Hatua Za Kisheria Wale Wote Watakaobainika Kwa Tuhuma Za Kuuza Damu. 

Aidha Njingo Amewaomba Wananchi Kuendelea Kujitokeza Katika Vituo Maalumu Kuchangia Damu Ili Kuwasaidia Watu Mbalimbali Wenye Mahitaji Ya Damu Kwa Lengo La Kuokoa Maisha Yao. 

KUNDAELI SARIA , AFISA UTUMISHI MPANGO WA DAMU SALAMA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI AKITOA MAELEZO KUHUSU MPANGO HUO KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO JUNI 14, 2012 OFISI KWAKE

 


WAKULIMA WANAOKOPA MATREKTA SUMA JKT KUPATA AHUENI


Na;Robert kakwesi,Igunga

WAKULIMA wanaokopa matrekta ya SUMA JKT,watakaopata majanga kama ukame,watafikiriwa kwa kutolipa mkopo kwa mwaka husika kwa vile so tatizo lao.

Akizungumza na wanachama wa chama kikuu cha ushirika cha Igembensabo,Meneja Mradi Kilimo Kwanza wa SUMA JKT,Kanali Felix Samillan amesema majanga yanajulikana yanapotokea na wakulima wanaokopa matrekta toka SUMA JKT wasiwe na wasiwasi kwani hilo litaangaliwa.

Ameeelza tatizo ni pale mkulima aliyekopa akikwepa kulipa deni wakati hana tatizo linalomkabili kwani huyo hataeleweka na lazima alipe deni.

Kanali Samillan ameeleza tayari serikali imeagiza matrekta yapatayo elfu tatu ambayo yatawasili muda wowowte hapa Nchini  na kuwataka wanachama wa Igembensabo kuyachangamkia yatakapowasili ili wawe na kilimo chenye tija kitakachowaondoa kwenye umaskini.

Awali meneja Mkuu wa Igembensabo.Bw.Emmanuel Malunde,alisema chama chake kimeomba kuwa wakala wa matrekta ya SUMA JKT ili wanachama wake wayapate kwa urahisi na kuyatumia kupambana na umaskini ombi ambalo lilipokelewa kwa furaha na Kanali Samillan aliyeitaka Igembensabo kutuma maombi rasmi.

Kanali Samillan alisema Igembensabo ni ushirika mkubwa unaotambulika na wanachama wake watajikomboa na kwamba ana uhakika wakikopa watalipa kwa wakati pasipo matatizo yoyote.

"NITAONDOA MAKUNDI NDANI YA CCM UYUI"-MUSSA NTIMIZI



Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Uyui mkoani Tabora,Bw.Mussa Ntimizi amesema kazi kubwa iliyoko mbele yake baada ya uchaguzi ni kuhakikisha anavunja makundi miongoni mwa wanachama ambayo amedai kuwa bado ni tatizo na yatachangia kwa kiasi kikubwa  kukizorotesha  Chama hicho.

Mussa Ntimizi ambaye alikuwa akiongea na mtandao huu ofisini kwake mjini Tabora,amesema amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwepo kwa mgawanyiko miongoni mwa wanachama akiwemo Mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini Mh.Shaffin Suma ambaye katika kipindi chote cha kampeni hadi uchaguzi alikuwa akimsaidia Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw. Abdallah Kazwika ambapo katika uchaguzi huo alishindwa na Bw.Mussa Ntimizi.

''Ninahitaji kuvunja makambi na kama tukiweza hili mengine yote yatakuwa rahisi ndani ya Chama chetu"alisema Mussa huku akiweza wazi kuhusu makundi hayo yanavyoendelea kujionesha wazi wakati wa hatua za mwanzoni tu za uongozi wake jambo ambalo amedai kutoliachia liendelee ndani ya CCM.

Katika kudhihirisha kuwepo kwa athari za makambi hayo yeye kama Mwenyekiti amejaribu mara kadhaa kumpigia simu Mbunge wa Tabora Kaskazini Mh.Suma kumuita katika kikao cha chama ambaye hakutaka kupokea simu hiyo....''Nilimpigia Mh.Suma kumwita kwenye kikao,mara ya kwanza alipokea na nilipojitambulisha kwake kwakuwa namba ya simu yangu alikuwa hana alipokea na kuikata,niliendelea kumpigia hakupokea kabisa na hatimaye akazima simu,jambo ambalo lilinifanya nitambue kuwa bado tatizo lipo kwakuwa nilipiga tena simu kwa siku iliyofuata hali ilikuwa ni ile ile kwa kiongozi huyo aliyepewa dhamana kubwa na wananchi ya kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Akiendelea kuzungumzia vipaumbele alivyojiwekea mara baada ya kuchaguliwa Ntimizi alisema mbali na kuvunja makambi hayo sasa ni wakati muafaka wa kusimamia kwa dhati Ilani ya CCM.

Na kuhusu suala la Kuwania Ubunge ifikapo mwaka 2015 Bw.Ntimizi alisema bado ni mapema mno kulizungumzia hilo.     

MAAFISA KILIMO,MIFUGO KUTOKA MIKOA YA KANDA YA KATI,MWANZA NA TABORA NA WAKULIMA WAPATA MAFUNZO YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI TABORA

Baadhi ya maafisa kilimo na mifugo kutoka mikoa ya kanda ya kati,Mwanza na Tabora pamoja na baadhi ya viongozi wa wakulima wakiwa katika mafunzo kwa vitendo wakati walipotembelea Ujenzi wa bwawa la maji la Inala linalotarajiwa kuendesha kilimo cha Umwagiliaji baada ya kukamilika.

 Uoneshaji wa ramani halisi ya ujenzi wa bwawa la Inala lililopo nje kidogo ya mji wa Tabora.

Mafunzo ya shughuli za umwagiliaji yanayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Veta mjini Tabora.

CCM YAPATA JEMBE LA UHAKIKA TABORA... NI JOHN MCHELE MJUMBE WA NEC

  Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele.

"Haikuwa rahisi kuamini kwamba hivi huyu John Mchele ndiye sasa ni mjumbe wa NEC ya CCM au ni utani"...Haya yalikuwa baadhi ya maneno ya wadau mbalimbali mjini Tabora kwa kuamini kuwa John Mchele ni mtu makini na ambaye akidhamilia kufanya jambo fulani na tena lililo na maslahi  kwa jamii huwa harudi nyuma hadi kupatikana kwa mafanikio au la sivyo jua litachomoza na kuzama hadi kieleweke.

Kwa wakati mwingine pia ilikuwa ni mshangao kwa baadhi yao ambao waliwahi kumshawishi hata kugombea Ubunge katika chaguzi zilizowahi kufanyika hasa wa mwaka 2000,2005 na 2010 lakini John Mchele hakuwa tayari kufanya hivyo na wala kuonesha dalili zozote za kujitosa katika kinyang'anyiro chochote ndani ya CCM kwa wakati huo.

Binafsi najaribu kujiuliza hivi John Mchele inawezekana kuwa kuna mtu alimshawishi kuingia kwenye ulingo wa siasa na kuacha Shughuli zake nyingine za kawaida?au amekwisha fikia uamuzi wa kuingia kwenye siasa kwa wakati huu ambao kumekuwa na mivutano ya mara kwa mara baada ya kuzuka kwa makundi ndani ya CCM?

Kwahili napingana nalo,kwakuwa John Mchele ninavyomfahamu si mtu wa makundi,si mtu wa kushawishiwa kuingia kwenye migogoro,na wala si mtu wa kulipizana kisasi na mtu aliyemkosea na kwa uthibitisho wa hili ni pale John Mchele alipowahi kushika nyadhifa mbalimbali za ngazi za mkoa hasa kwenye vitengo vya Taasisi za wafanyabiashara na wasafirishaji,jambo ambalo ilidhihirika kuwaunganisha wanachama katika Taasisi hizo na Serikali hatua ambayo iliondoa migongano iliyokuwa imedumu kwa muda mrefu pasipo ufumbuzi.

Na hata nilipojaribu kungia mitaani ili nipate sifa mbaya ya John Mchele, napo niligonga mwamba baada ya kila mmoja niliyebahatika kuzungumza naye alinihakikishia kuwa John Mchele ni Mjamaa wa Kweli kwa shida na raha,...."Anashiriki kwa hali na mali shughuli za kijamii mitaani,Ukiwa na shida binafsi hata kama hana uwezo wa kukusaidia ujue atakupa hata ushauri ambao utakusaidia kuondokana na dhahama iliyokukumba"ni maneno ya mmoja kati ya watu wa mjini Tabora.

HIVI KWANINI JOHN MCHELE KACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA NEC YA CCM
Hapa sioni sababu ya kufikiria sana kwani kwa haya yote niliyokumbana nayo huko mtaani,maofisini na hata kwa wafanyabishara Sokoni, naamini CCM kwa umakini wake huko Dodoma iliamuliwa kati ya majina matano yaliyorudi ni pamoja na la John Mchele baada ya kupimwa na kikao kizito ambako vigogo ngazi ya juu wa CCM Taifa walifanya maamuzi hayo.

Sitaki kuzungumzia uchaguzi uliomuweka katika nafasi hiyo ya ujumbe wa NEC ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha utumishi wa Umma au Uhazili ambako kulikuwa na patashika ingawa nguo hazikuchanika John Mchele akaibuka mshindi hata sasa kwa hatua hiyo anaanza kutambulika kuwa ni kiongozi halali ngazi ya juu ya CCM ingawa wapo watu hawakupenda litokee hilo.

Jitihada zake katika kuonesha ni jinsi gani naye anaweza kuwaongoza  wana CCM wenzake na hasa mchango wake makini unahitajika sana wakati huu wa mfumo wa vyama vingi kwakuwa ili CCM iweze kushinda inahitaji ipate watu wabunifu,Waaminifu na Waungwana kama John Mchele na hasa inapofikia wakati wa Uchaguzi mkuu nchini.

Lakini pia nikirudi nyuma nazidi kuufikiria uvumi ambao umezagaa mkoa mzima wa Tabora,Eti wanaCCM wenyewe wanasema muda umefika wa kuwapa Uongozi watu ambao wanaishi yaani WANALALA NA KUAMKA WAKIWA TABORA na si wale WANAOISHI DAR-ES-SALAAM WANAKUWA WAKARIMU SANA WAKATI WANAPOKUJA TABORA KUTAFUTA UONGOZI na baada ya hapo maisha yao ni Dar-es-Salaam.

"Kwakweli tunazidi kudharaulika sana utadhani hapa hakuna watu kabisa wanaoweza kuongoza!,sasa tumechoka,tunawaambia walioko nje ya Tabora....HAPA SIO SHAMBA LA BIBI"....Haya sio maneno yangu ni wadau wa Tabora hao wameamua kufunguka.

Maamuzi ya John Mchele kuamua kujitosa katika kinyang'anyiro hicho ulipokelewa kwa Shangwe na wanaCCM waliowengi na kuweza kumuhakikishia John aone kuwa kumbe hata mtu asiyefahamika na wengi na tena ambaye hajawahi kugombea nafasi yoyote katika Chama anaweza kuwa kiongozi na akafanya vitu zaidi ya yule ambaye ana jina kubwa na fedha kibao.

"NAWAPONGEZA  WOTE WALIONICHAGUA NA WASIO NICHAGUA KWANI WAMETUMIA DEMOKRASIA YA KWELI"...Hayo ni maneno ya John Mchele huku akisisitiza kuwa na umoja miongoni mwa wanaCCM wote. 
     

MUSSA NTIMIZI MWENYEKITI MPYA CCM UYUI,...DK.MFUTAKAMBA AANGUKA UJUMBE WA NEC

UCHAGUZI wa CCM wilaya ya Uyui mkoani Tabora,umekamilika jana,huku
uenyekiti ukiangukia kwa Musa Ntimizi, akimshinda mwenyekiti wa zamani
Abdalah Kazwika.
Musa Ntimizi ni mtoto wa mbunge mstaafu wa jimbo la Igalula,Tatu Ntimizi.

Wakati hayo yakijiri,mbunge wa jimbo la Igalula Dkt Athuman Mfutakamba
alijikuta kwenye wakati mgumu pale alipoangukia pua kwa kushindwa kiti
cha NEC huku akipigwa swali zito ambalo lilionekana kummaliza.

Dkt Mfutakamba wakati akijieleza mbele ya wajumbe aliulizwa ni vipi
anataka ujumbe wa NEC ilihali unaibu waziri wa Uchukuzi ulimshinda na
rais Jakaya Kikwete akamuondoa.
Katika majibu yake Dkt Mfutakamba alijibu kuwa siyo kwamba alishindwa
kazi na rais akamuondoa bali tuhuma dhidi yake zilikuwa za kupikwa
namajungu tu.

Awali uchaguzi huo wakati umeshafanyika na kura zinahesabiwa,naye
mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini Shaffin Sumar, majira ya saa
10:08,aliwashangaza wajumbe wa mkutano baada ya kutoka ndani ya chumba
cha kuhesabia kura kwa hasira akidaiwa kuona upepo mbaya kwa mtu wake
ambapo alipanda gari yake na kuondoka na hakurudi tena hadi matokeo
yanatangazwa.

Shaffin Sumar inadaiwa kuwa ni mfuasi wa mwenyekiti aliyeshindwa
kwenye kinyang`anyiro hicho,Abdalah Kazwika na alikuwa akimfanyia
kampeni kubwa kiasi cha kuzua malalamiko toka kwa wagombea wengine
ambao waliandika barua za malalamiko.

Aidha katika uchaguzi huo ulioanza majira ya saa 12:20 mchana,matokeo
yake yalitangazwa saa 07:03 usiku.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo,mstahiki meya wa
manispaa Tabora,Ghulamdewji Remtulah alisema mshindi wa nafasi ya
mwenyekiti ni Musa Ntimizi, aliyepata kura 769,akifuatiwa na
mwenyekiti wa zamani Abdalah Kazwika aliyepata kura 544,na Hamis
Bundala, alipata kura 26 na kura zilizopigwa ni 1,412 na
zilizoharibika ni 24.

Remtulah alitangaza pia matokeo ya nafasi ya ujumbe wa NEC,ambapo
afisa mtendaji wa kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui,Beatus Mlolwa
alishinda kwa kishindo kwa kupata kura 706 akimshinda mbunge wa jimbo
la Igalula, Dkt Athuman Mfutakamba akiambulia kura 231,na Shija Humbi
kura 200 na kura zilizopigwa ni 1,359 na zilizoharibika ni kura 51.

Aidha katika nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu mkoa,washindi walikuwa
watano ambapo Joseph Kidaha alipata kura 873,akifuatiwa na mke wa meya
wa zamani wa jiji la Dar-es-Salaam,Kitwana Kondo,Hanifa Kondo, kura
852,James Januari kura 487,Msafiri Abduhamad kura 449, naDavid
Malicela kura 385, na kurabzilizopigwa zilikuwa ni 1,433.

Akishukuru wajumbe wa uchaguzi huo,mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya
Uyui,aliwashukuru wajumbe hao na kuahidi kutokomeza makundi yote na
kwamba kila mwanachama hadi sasa ni wake.

“Nitashirikiana na wanaCCM wenzangu sina kinyongo na wote ambao
hawajanipigia kura CCM ni ya wote kamwe sitabagua wala kuendekeza
makundi ambao yanakibomoa chama chetu.” alisema Ntimizi.

Aidha taarifa ambazo hazijathibitishwa na katibu wa CCM wilaya ya
Uyui,Flavian Wangwe zinasema Dkt Athuman Mfutakamba, amewasilisha
malalamiko akidai amechakachuliwa.
Hata hivyo gazeti hili lilimshuhudia Dkt Mfutakamba, akiwa nje ya
ofisi ya CCM Uyui akilalalama kuwa alichezewa faulu hakuwa mtu wa
kushindwa kiti cha NEC.

CCM TUTASHINDA RUFAA


 Na Lucas Raphael,Igunga
 
CHAMA Cha Mapinduzi CCM wilayani Igunga mkoani Tabora kimethibitisha kukata rufaa na kuwasilisha hoja katika mahakama kuu ya rufaa.
 
Hayo yalisemwa na katibu wa chama hicho wilaya Mery Maziku kuwa chama hicho tayari kimewasilisha hoja mbadala za kupinga maamuzi ya mahakama kuu kanda ya tabora yaliyo tengua ubunge wa Dkt,peter kafumu aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga.
 
Akizungumuza katika mkutano MKuu wa wilaya wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Hospital ya mission Nkinga katibu huyo alisema kuwa maamuzi yaliyofan ywa na mahakama ya kanda hayakuzingatia ukweli wa hoja zilizo pelekwa na mlalamikaji.
 
Alisema kuwa kwakuwa haki haikuishia hapo chama hicho kimejipanga kusimama tena katika mahakama ya rufaa ili kutafuta haki ya ubunge wa kafumu.
 
‘’Maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya kanda hayana msingi lakini tunaheshimu sana ndio maana tumejipanga kukata rufaa na leo tumekamilisha hoja zetu zote hapo mahakamani lazima tutashinda kwani hoja zetu ni za msingi’’alisema katibu huyo.
 
Katibu huyo alipoulizwa ni hoja ngapi walizo ziwasilisha katika mahakama hiyo ya rufaa hakuweza kutoa jibu na badala yake alisema kuwa mpka hapo baadae atakapo pata muda wa kwenda ofisini.
 
Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dkt,Peter kafumu akito shukrani mara baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa halmashauri kuu taifa Nec alisema kuwa kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa nifursa ya pili ya kuwatumikia wananchi wa Igunga.
 
Alisema kuwa kwa kuwa amechaguliwa atahakikisha anawatumikia wananchi wa Igunga na wanachama wa chama hicho ili kuendeleza ahadi zake ambazo alikuwa amweziahidi wakati akiwa mbunge.
 
Akizungumzia rufaa ya mahakama kuu katika ukumbi huo alisema kuwa chama kimekata rufaa  ilikuhakikisha haki inapatikana ili arudi kuwa tumikia wananchi wa Igunga kama mbunge wa jimbo hilo .
 
Nina imani na rufaa hiyo iliyokatwa na chama hivyo tutashinda nanitarudi kuwa tumikia wananchi wa Igunga kama mbunge wao tena lazima tutashinda kwani hoja zilizo wasilishwa ni za msingi.
 
Katika uchaguzi huo aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho Fericx Mkunde alikiachia kiti hicho kwa mwenyekiti mpya Coaster Olomi huku nafasi ya pili ya pili ikichukuliwa na fericx mkunde.
 
Katika wilaya ya sikonge aliyekuwa akitetea kiti hicho Abisai Razalo Mboga ameibuka kitedea huku nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa Nec ikichukuliwa na mbunmge wa jimbo hilo  said Juma Nkumba.
 
Mwisho.