Na Lucas Raphael,Igunga
CHAMA
Cha Mapinduzi CCM wilayani Igunga mkoani Tabora kimethibitisha kukata rufaa na
kuwasilisha hoja katika mahakama kuu ya rufaa.
Hayo
yalisemwa na katibu wa chama hicho wilaya Mery Maziku kuwa chama hicho tayari
kimewasilisha hoja mbadala za kupinga maamuzi ya mahakama kuu kanda ya tabora
yaliyo tengua ubunge wa Dkt,peter kafumu aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga.
Akizungumuza
katika mkutano MKuu wa wilaya wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Hospital
ya mission Nkinga katibu huyo alisema kuwa maamuzi yaliyofan ywa na mahakama ya
kanda hayakuzingatia ukweli wa hoja zilizo pelekwa na mlalamikaji.
Alisema
kuwa kwakuwa haki haikuishia hapo chama hicho kimejipanga kusimama tena katika
mahakama ya rufaa ili kutafuta haki ya ubunge wa kafumu.
‘’Maamuzi
yaliyotolewa na mahakama ya kanda hayana msingi lakini tunaheshimu sana ndio maana
tumejipanga kukata rufaa na leo tumekamilisha hoja zetu zote hapo mahakamani
lazima tutashinda kwani hoja zetu ni za msingi’’alisema katibu huyo.
Katibu
huyo alipoulizwa ni hoja ngapi walizo ziwasilisha katika mahakama hiyo ya rufaa
hakuweza kutoa jibu na badala yake alisema kuwa mpka hapo baadae atakapo pata
muda wa kwenda ofisini.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo
Dkt,Peter kafumu akito shukrani mara baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa
halmashauri kuu taifa Nec alisema kuwa kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa
Halmashauri ya chama hicho taifa nifursa ya pili ya kuwatumikia wananchi wa
Igunga.
Alisema
kuwa kwa kuwa amechaguliwa atahakikisha anawatumikia wananchi wa Igunga na
wanachama wa chama hicho ili kuendeleza ahadi zake ambazo alikuwa amweziahidi
wakati akiwa mbunge.
Akizungumzia
rufaa ya mahakama kuu katika ukumbi huo alisema kuwa chama kimekata rufaa
ilikuhakikisha haki inapatikana ili arudi kuwa tumikia wananchi wa Igunga kama
mbunge wa jimbo hilo
.
Nina
imani na rufaa hiyo iliyokatwa na chama hivyo tutashinda nanitarudi kuwa tumikia
wananchi wa Igunga kama mbunge wao tena lazima
tutashinda kwani hoja zilizo wasilishwa ni za msingi.
Katika
uchaguzi huo aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho Fericx Mkunde
alikiachia kiti hicho kwa mwenyekiti mpya Coaster Olomi huku nafasi ya pili ya
pili ikichukuliwa na fericx mkunde.
Katika
wilaya ya sikonge aliyekuwa akitetea kiti hicho Abisai Razalo Mboga ameibuka
kitedea huku nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa Nec ikichukuliwa na
mbunmge wa jimbo hilo
said Juma Nkumba.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment