Friday, October 5, 2012

MARUKUFUKU DAMU KUUNZIWA WAGONJWA NCHINI






Wananchi Mkoani Tabora Wametakiwa Kuwafichua Watumishi Wa Afya Ambao Wanaowauzia.

Wagonjwa Damu Hospitalini Badala Ya Kutolewa Bure Ili Waweze Kuchukuliwa Hatua Za Kisheria Kwa Lengo La Kukomesha Tabia Hiyo.
 
Wito huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha  maabara katika benki ya Damu salama mkoa wa Tabora ,Thomas Njingo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana baada ya kutokea kwa wananchi kulalamika kuuziwa damu .
 
Alisema Wananchi Wakishikamana Pamoja Katika Kuwafichua Watumishi Wa Afya Wanaowauzia Wagonjwa Damu Inayotakiwa Kutolewa Bure Ni Dhahiri Kuwa Vitendo Hivyo Vitakomeshwa Na Wananchi Wataipata Huduma Hiyo Pasipo Usumbufu. 

Amefafanua Kuwa Kitendo Cha Wananchi Kuuziwa Damu Hospitalini Kinachangia Kwa Kiasi Kikubwa Watu Kukosa Imani Nao Hali Inayosababisha Washindwe Kuwa Na Mwamko Wa Kuchangia Damu Kwa Hiari Pindi Wanapotakiwa Kufanya Hivyo.

Njingo Amesema Damu Hiyo Ambayo Wananchi Huchangia Inapaswa Kutolewa Bure Kwa Wagonjwa Wakiwemo Wajawazito, Majeruhi Wa Ajali Mbalimbali Pamoja Na Watoto. 

Mkuu Huyo Wa kitengo cha  Maabara Amewasihi Wananchi Kutoa Taarifa Sehemu Husika Ikiwemo Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa- Takukuru Pindi Wanapoona Wagonjwa Wao Wanauziwa Damu Inayopaswa Kutolewa Bure Na Kwamba Hawatasita Kuwachukulia Hatua Za Kisheria Wale Wote Watakaobainika Kwa Tuhuma Za Kuuza Damu. 

Aidha Njingo Amewaomba Wananchi Kuendelea Kujitokeza Katika Vituo Maalumu Kuchangia Damu Ili Kuwasaidia Watu Mbalimbali Wenye Mahitaji Ya Damu Kwa Lengo La Kuokoa Maisha Yao. 

KUNDAELI SARIA , AFISA UTUMISHI MPANGO WA DAMU SALAMA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI AKITOA MAELEZO KUHUSU MPANGO HUO KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO JUNI 14, 2012 OFISI KWAKE

 


No comments:

Post a Comment