Friday, October 5, 2012

WAKULIMA WANAOKOPA MATREKTA SUMA JKT KUPATA AHUENI


Na;Robert kakwesi,Igunga

WAKULIMA wanaokopa matrekta ya SUMA JKT,watakaopata majanga kama ukame,watafikiriwa kwa kutolipa mkopo kwa mwaka husika kwa vile so tatizo lao.

Akizungumza na wanachama wa chama kikuu cha ushirika cha Igembensabo,Meneja Mradi Kilimo Kwanza wa SUMA JKT,Kanali Felix Samillan amesema majanga yanajulikana yanapotokea na wakulima wanaokopa matrekta toka SUMA JKT wasiwe na wasiwasi kwani hilo litaangaliwa.

Ameeelza tatizo ni pale mkulima aliyekopa akikwepa kulipa deni wakati hana tatizo linalomkabili kwani huyo hataeleweka na lazima alipe deni.

Kanali Samillan ameeleza tayari serikali imeagiza matrekta yapatayo elfu tatu ambayo yatawasili muda wowowte hapa Nchini  na kuwataka wanachama wa Igembensabo kuyachangamkia yatakapowasili ili wawe na kilimo chenye tija kitakachowaondoa kwenye umaskini.

Awali meneja Mkuu wa Igembensabo.Bw.Emmanuel Malunde,alisema chama chake kimeomba kuwa wakala wa matrekta ya SUMA JKT ili wanachama wake wayapate kwa urahisi na kuyatumia kupambana na umaskini ombi ambalo lilipokelewa kwa furaha na Kanali Samillan aliyeitaka Igembensabo kutuma maombi rasmi.

Kanali Samillan alisema Igembensabo ni ushirika mkubwa unaotambulika na wanachama wake watajikomboa na kwamba ana uhakika wakikopa watalipa kwa wakati pasipo matatizo yoyote.

No comments:

Post a Comment