Tuesday, December 31, 2013

MWAKASAKA AIPIGA TAFU TIMU YA NETBALL TABORA,AKABIDHI ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MBILI


Mlezi wa Chama cha Netball mkoa wa Tabora Emmanuel Adamson Mwakasaka akikabidhi zaidi ya shilingi milioni mbili kwa Katibu wa Chama hicho ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu ya Netball ya mkoa wa Tabora ambayo inashiriki michuano ya Taifa ya mchezo huo,fedha hizo ambazo zitasaidia nauli ya kwenda jijijni Dar-es-salaam ambako mashindano hayo yanafanyika.
Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiaga timu hiyo katika hotel ya Wilca mjini Tabora ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wachezaji wa timu hiyo kujiamini wakiwa mchezoni hatua ambayo itasaidia kuwapatia ushindi ambao utarejesha heshima ya mkoa wa Tabora kutokana na mchezo huo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Netball ya mkoa wa Tabora.

Mwakasaka ambaye pia ni mdau wa michezo mkoani Tabora alitumia fursa hiyo kuwaahidi wanamichezo hao kuwapa ushirikiano katika kuendeleza mchezo wa Netball huku akiwataka wachezaji kumuunga mkono kwa kufanya vizuri katika michuano ya Taifa wanayoshiriki  sasa.
Mdau wa mchezo wa Netball Hamisi Msoga naye alipata fursa ya kumkabidhi Mwakasaka mchango wa shiriki 50000/= kwa ajili ya kusaidia timu hiyo ya Netball.
Kiongozi wa timu ya Netball ya mkoa wa Tabora ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Tabora Suleimani Kumchaya wakati akitoa hotuba ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo.

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KULA UYOGA

Na Lucas Raphael,Urambo

 

WATU watatu wamefariki dunia baada ya kula mboga aina ya uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu wilayani Urambo mkoani Tabora.

Alizungumza na waandishi wa habari katika hospital ya wilaya ya urambo, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk.Kheri Kagya,alisema kwamba  watu hao walikuwa wanane na walikula ugali kwa mboga aina ya uyoga ambao unadhaniwa kuwa na sumu katika kijijini Igunguli, katika Kata ya Uyogo wilayani humo.

alisema kwamba mmoja wa wazazi katika familia hiyo Makoye Tongele (35) aliamua kuwapeleka Hospitali ya wilaya ya Urambo, watoto Kija Makoye (3) aliyefariki njiani na Wande Mahinge (5) na Mahigi Tongele waliofariki wakipata matibabu katika Hospitali hiyo. 

 
 Dk. Kagya alibainisha kuwa wengine waliokula chakula hicho walisalimika akiwemo Baba wa watoto hao Makoye pamoja na watoto wengine Gimili Makoye(miezi kumi) na Talekwa Mahigi(3) akiwemo pia aliyepika chakula hicho Nyanzobe Mswahili(25).

Dk.Kagya alisema wameshindwa kuchukua sampuli ya chakula hicho kinachohisiwa kuwa na sumu kwa vile kililiwa chote na hata aina ya uyoga wameshindwa kuutambua kwa vile nao ulichumwa wote.

Ameeleza kuwa Nyanzobe aliwaeleza kuwa uyoga aliochuma  porini ulikuwa unafanana na uyoga waliowahi kula na hivyo kukwama kuutambua uyoga huo.

Kamamda wa Polisi Mkoani Tabora,Kamishna Msaidizi wa Polisi Peter Ouma alisema wamepata taarifa za tukio hilo na kusisitiza kwamba wananachi kuwa waangalifu kipindi hiki cha masika kwani uyoga nyingi zinaota kutokana na rutuba zilizopo maeneo mbalimbali kwa ajili ya mvua zinazonyesha mkoani hapa

Hata hivyo aliwataka wananchi wanaopenda mboga aina hiyo kuchukua tahadhari ili wasikutane na mboga aina ya  uyoga wenye sumu kama huo .

mwisho-

Sunday, December 29, 2013

WAATHIRIWA WA MAFURIKO TABORA WAPATA MSAADA WA UNGA WA MAHINDI


Baadhi ya waathiriwa wa mafuriko yaliyotokea hivi katika  kata za Malolo na Chemchem zilizopo manispaa ya Tabora wakisubiri mgawo wa msaada wa Chakula kilichotolewa na Ofisi ya halmashauri ya manispaa ya Tabora kufuatia nyumba zao kukumbwa na mafuriko hayo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na Chakula na hivyo Serikali kuamua kutoa msaada huo kwa waathiriwa zaidi ya 102. 
Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij akikabidhi msaada wa Chakula kwa diwani wa Kata ya Malolo Bi.Zinduna Kambangwa kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mjini hapa ,ambapo makabidhiano hayo yalifanywa mbele ya Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya,Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda ambapo msaada huo ni tani moja na robo ya unga wa mahindi. 
Baadhi ya Waathiriwa wa mafuriko hayo wakisaidiana kubeba unga ambao ni kilo 25 walizopatiwa kila mmoja.

MAFURIKO YAPIGA HODI TABORA MJINI,FAMILIA KADHAA ZAKOSA MAKAZI


Baadhi ya watoto ambao wanaishi katika nyumba zilizokumbwa na mafuriko eneo la Kata ya Malolo manispaa ya Tabora,watoto hawa walifanikiwa kuokolewa na hivyo wamelazimika kukaa nje ya nyumba zao wakisubiri maji yapungue. 

Mmoja kati ya akina mama wakazi wa Malolo akitafuta baadhi ya vyombo vya kupikia ambavyo vilisombwa na maji wakati wa mafuriko hayo ambayo yamesababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamekosa makazi na kuhifadhiwa kwenye nyumba za jirani ambazo hazikukumbwa na mafuriko hayo yaliyoanza majira ya saa moja na nusu asubuhi kufuatia mvua za masika zinazoendelea kunyesha mjini Tabora.
Nyumba ya mchungaji wa kanisa la Injili Afrika  Elias Mbagata iliyoko kata ya Malolo manispaa ya Tabora nayo ilikuwa ni moja kati nyumba zilizokumbwa na adha hiyo.
Nyumba hizi zilikumbwa na mafuriko hayo.
Kamanda wa Polisi  wilaya ya Tabora mjini Bw.Samwel Mwampashe akiwa eneo la Mafuriko kata ya Malolo ambapo nyumba kadhaa zilikumbwa na mafuriko hayo lakini imeripotiwa kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya uharibifu wa vifaa na mali mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya,Mkurugenzi wa manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda pamoja na Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij walifika kushuhudia mafuriko hayo yaliyotokea kata ya Malolo na kusababisha familia kadhaa kukosa mahali pa kuishi. 


Saturday, December 21, 2013

WATOTO WANAOHISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WAPATIWA MSAADA



  NA LUCAS RAPHAEL TABORA

Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya  Tabora Christian Youth Network imetoa wa  maada wa vifaa vya shule kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi katika kata za kakola, Uyui na Gongoni katika wilaya ya tabora .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ,Adriano Kalisti, alisema kuwa kwa ufadhili wa shirika la kimarekani liitwalo SAVE AFRICAN’S CHILDREN .
Alisema kwamba shirika hilo limekuwa litoa huduma za vifaa vya shule kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi kama vile madaftari na kalamu.


Alisema kwamba kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto waishio na virusi vya ukimwi na walioathiriwa wapato 75 na  kuanzisha clubs maalumu zinazowakutanisha watoto hao kila mwezi kwa ajili ya kupata elimu ya afya, kupata huduma za kisaikolojia kwa kucheza michezo mbalimbali.

Alisema kuwamba  changamoto mbalimbali wanazopitia kulingana na hali zao pamoja na kupata chakula cha pamoja chenye lishe kwa ajili ya ujengaji wa afya zao.


Kalist alisema  kuwa wanakusudia kusaidia jumla ya watoto 500 katika kipindi cha miaka mitatu yaani 2013-2016  katika maeneo ya kuwajengea walezi/wazazi wao kiuchumi, Afya, elimu, ulinzi na kutoa msaada wa kisaikolojia.


Alisema mnamo mwezi January 2013 CYN inajarajiwa kuendesha program maalumu ya kukusanya watoto zaidi ya 300 ili luwashirikisha, upendo, Furaha kwa kula chakula cha pamoja, kucheza michezo mbalimbali, kuwezesha watoto kutoa hisia zao kwa jamii juu ya matatizo wanayopitia.


Alisema kuwa wanatarajia kuzindua kampeni maalumu ijulikanayo kwa jina la “ HURUMIA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KATIKA ENEO LAKO, BEBA MZIGO” Kampeni hii imelenga kuhamasisha jamii kuwa na moyo wa dhati/ mzigo wa kusaidia watoto waishio katika mazingira katarishi katika maeneo waishio bila kutegemea wahisani.


Alisema kwamba shirika la Christian Youth Network inakaribisha wadau wengine kama vile makampuni na watu binafsi katika kudhamini shughuli hii muhimu inayotarajiwa kufanyika Mwaka mpya 2014 katika tarehe za mwanzoni.

Mwisho

UKATILI WA KIJINSIA TABORA:-MGANGA WA KIENYEJI AMVUNJA TAYA MKEWE!


Mariam Crispin Kilimba(52)mkazi wa Ipuli manispaa ya Tabora anayedaiwa kupigwa na mumewe Bw.Himid Hassan Kitebo(58)ambaye ni mganga wa Kienyeji na kusababisha kumvunja taya. 
Bi.Joha Aman(38)mkazi wa kata ya Isevya alipigwa na mumewe na kujeruhiwa vibaya ambapo amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Tabora bado yanaendelea kushika kasi siku hadi siku.

AJALI YA LORI YAUA WANNE YAJERUHI ZAIDI YA 30-TABORA



 

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma akiangalia Lori aina ya Isuzu lenye nambari za Usajili T829 AHH mara baada ya kuanguka na kusababisha vifoo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 30 katika ajali iliyotokea Tarafa ya Ilolangulu wakati lilipokuwa likienda mnadani huku likiwa limebeba wafanyabiashara wa mitumba pamoja na mizigo mbalimbali.
Tairi la Lori hilo ambalo lilikuwa bovu lilipasuka na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Dereva wa Lori hilo Isuzu Bw.Ally Athuman ambaye alikutwa eneo la ajali hiyo mbaya
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la ajali wakishuhudia Maiti zilizokuwa zimekusanywa kwenye gari la Polisi muda mfupi mara baada ya ajali kutokea.
Madaktari chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani Tabora wakijaribu kuandika majina ya watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa.
Kikosi maalumu cha huduma ya kuokoa afya ya majeruhi katika hospitali ya Kitete ambacho kilichukua hatua za haraka na makusudi kushughulikia majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo.
Idadi kubwa ya watu walivunjika miguu na mikono mbali na wale waliopoteza maisha ambao majeraha makubwa walipasuka vichwa na kuumia vifuani.


Friday, December 20, 2013

WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 120



Na Lucas Rphael,Nzega


MAHAKAMA ya Hakim mkazi wilayani Nzega Mkoani Tabora imewahukumu watu wa wa 4 kwenda jela miaka 120 kutokana na kukutwa ha hatia ya kufanya unyan`ganyi kwa kutumia silaha.

Waliotiwa hatiwa hatiani na mahakama hiyo ya  hakimu mkazi  ni  ,Joseph Manala(38),Emmanuel machibya(20)Juma Lutalamula(30)Juma msabato(42).

Akisoma hukumu hiyo hakim mkazi wilaya ya nzega, Silvester Kainda watuhumiwa wa nne (4)  wametiwa hatiani kwa kosa la kuvamia kwa kutumia siraha na kupewa hukumu ya miaka 120 huku kila mmoja akitumikia miaka 30 gerezani.

Alisema kwamba vitendo vya unyan`ganyi kwa kutumia silaha vimekuwa vikiongezeka kila siku jamboo ambalo linatishia amani ya watanzania hivyo dhahabu kali ndio lilio sahii kwa watu waina hii.

Alisema kwamba hiyo iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kupara mali zawatu ambao wametafuta kwa jasho lao na wengine kuchukua mali hizo kama zao..

Hakimu kainda aliiambia mahakama hiyo kwamba ushidia uliotolewa mahakani hapo umeonyesha bila shaka na kufanya mahakamni iweze kuwatia hatiani washitakiwa hao kwani nikweli walitenda kosa hilo  .

Hata hivyo mahakama hiyo imewaachia huru watuhumiwa wawili baada ya kuonekana kutokuwa na hatia katika shitaka hilo kuwa ni Peter Steven (30) pamoja na Ramadhani Juma (19).

Awali mwendesha mashitaka wa Jeshi la polis wilaya Melito Ukongoji aliiambia mahakama  hiyo kuwa mnamo April 5 mwaka huu katika cha  kijiji cha Itanana kata ya Bukene walikuiba Duka la Joakim John mkazi wa kijiji hicho kisha na kumjeruhi vibaya mwili wake.


Mwendesha  akisoma shitaka hilo alisema kuwa watuhumiwa hao waliiba fedha zaidi ya laki saba na kufanya uhalibifu mkubwa wa mali ikiwa na kumjeruhi Joakim John huku wakitumia siraha aina Gobole na mapanga.

Kabla ya kutolewa kwa hukum hiyo mwendesha mashitaka Melito aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa watuhumiwa hao kutokana na kukithiri kwa matukio hayo ili iwe fundisho kwa watu kama hao.

Wakati wa kujitetea watuhumiwa hao waliiomba mahakama hiyo itoe hukum ndogo kutokana na baadhi yao kuwa ni waathirika wa Virusi vya ukimwi huku wengine wakikabiliwa na majukum ya kifamilia.





Mwisho.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI TABORA


Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda akizungumza na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu ya Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Tabora TBPC,kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Theonas Liwa,anayefuata ni Katibu wa chama hicho Bw.William Mahimbo na Vivian Pyuza ambaye ni Mwekahazina mkuu wa TBPC.Mkurugenzi huyo alitembelea ofisi ya chama hicho na kushauri mipango ya maendeleo ya TBPC ikiwa ni pamoja na kuwataka viongozi hao kuomba kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi kubwa.   
Mkurugenzi huyo wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Alfred Luanda ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea ofisi ya klabu ya Waandishi wa habari Tabora ambapo uongozi wa ulimweleza changamoto kadhaa zinazoikabili klabu hiyo yenye wanachama wasiopungua 32.

MSANII WA UGANDA ZIGGY DEE KUACHIA NGOMA MPYA YA KIHISTORIA TABORA "LIVINGSTONE CITY"

Friday, November 29, 2013

Ziggy Dee msanii toka Uganda aliyetamba na Eno Mic akiwa studio za Kapestone-Tabora
Producer EiZeR BiT kwenye mashine
Kushoto: Producer EiZeR BiT, Ziggy Dee na Pro. BK mavinanda.
Wadau wa ukweli kwa pozi
Appson, Ziggy Dee na Stone Wa Kitaa [wa kulia] - wote wasanii
Ziggy Dee na Ma-Producer wake.

Na Lucas Raphael,Tabora.
Ziggy Dee, ambaye ni msanii pekee wa Afrika mashariki na kati  akiwa ni mara yake ya kwanza kuingia katika mkoa wa Tabora na kufanya wimbo unaousifia mkoa huo.
Katika wimbo wake huo aliouita kwa jina LIVINGSTONE CITY msanii huyo nguli wa muziki wa kizazi kipya  amedai kuwa kihistoria katika vitabu vinavyosomwa kwingineko duniani kote, Tabora imekuwa ni sehemu maarufu kama moja ya njia na kituo  cha biashara ya utumwa enzi za ukoloni wa waarabu na waingereza.
Ziggy ambaye ameweka wazi kuwa  na Tabora ikiwa ni moja ya Trade routes maarufu,ambayo mmoja kati ya viongozi wa wakoloni  Dr. David Livingstone alipita na kuweka himaya yake enzi hizo za harakati za kutokomeza biashara ya utumwa  iliyokuwa ikifanywa na dola ya  Waarabu,hatua ambayo inazidi kuimarisha historia ya mkoa wa Tabora na kufanya ni moja ya vivutio vya utalii kwa maliasili za kale zinazotokana na mabaki au masalia ya majengo,njia za watumwa na vitu mbalimbali vya asili ya Mwafrika.

Licha ya historia ya pekee ya mkoa wa Tabora iliyouwekea ramani ya dunia katika masuala ya utalii wa mali za kale, msanii huyu Ziggy amezungumzia kuwa haijalishi kuwa yeye ni  raia wa Uganda lakini akaweka bayana kuwa Afrika ni moja na Waafrika wote ni ndugu wanaostahili kujivunia tunu hiyo ya uwepo wa historia kubwa isiyo na mfano huku akidai kufurahishwa kwake kufika mkoa wa Tabora kwa mara ya kwanza baada ya kupafahamu kupitia  historia zilizoandikwa kwenye vitabu mbalimbali na hatimaye yeye pia kufika kwake atakuwa ameandika historia ya pekee na hasa kuandaa wimbo huo maalumu LIVINGSTONE CITY ambao pia ataufanyia video kabla ya kurejea nyumbani nchini Uganda.

Aidha kazi nzima ya kurekodi wimbo huo  imefanywa katika studio za hapahapa mkoani Tabora ifahamikayo kama KAPESTONE chini ya uongozi wao Ma-Producer  EiZeR BiT na BK (Baraka mavinanda). Ngoma hiyo ina mahadhi ya Raga na inatarajiwa kutambulishwa mapema hivi  karibuni.


DR.SLAA AWATAKA WANATABORA KUAMKA WAKATI RASILIMALI ZA TAIFA ZINATAFUNWA!!!


Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dr.Willibroad Slaa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Tabora uliofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui.
Baadhi ya wananchi wa mjini Tabora ambao walihudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema pamoja na bibi huyo hakuwa nyuma kusikiliza Dkt slaa .

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora Bw.Kansa Mbaruku akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wafuasi wa Chadema wakiwa katika mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui mjini Tabora.
Gari la Katibu mkuu wa Chadema Dr.Willibroad Slaa likiwa na ulinzi mkali likiondoka viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui mjini Tabora.

Wednesday, December 18, 2013

SOKO LA HISA LA DAR-ES-SALAAM LAPIGA HODI KWA WAFANYABIASHARA MKOANI TABORA


Meneja Miradi wa  Soko la hisa la Dar-es-Salaam  Bw.Magabe Maasa na meneja mkuu wa soko la hisa la dar Juventus Simon akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Tabora wakati wa ufafanuzi wa malengo ya Soko la hisa la Dar-es-salaam lilivyoamua kutembelea mikoa mbalimbali nchini kwa lengo kufanya Semina kwa wafanyabiashara kuhusu faida za uwekezaji kupitia ununuzi wa hisa kwenye mashirika na makampuni makubwa nchini.
Mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani Kumchaya aliyevaa miwani mstari wa mbele akiwa na maafisa wa Soko la hisa la Dar-es-salaam DSE pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wakati wa semina ya siku mbili iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Eagle mjini Tabora.

Wednesday, December 4, 2013

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SHIRIKA LA PSI TANZANIA KWA MKOA WA TABORA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI KWA MWAKA 2013.


KAIMU MKUU WA WILAYA YA URAMBO SAVERI MAKETA AKISIKILIZA VIONGOZI WA PSI WALIOPO PICHA JUU YA KAZI WANAZIFANYA KUELIMISHA JAMII JUU YA SWALA ZIMA LA KUTOA ELIMU YA UKIMWI MKOANI TABORA





Utangulizi:-


Psi – Tanzania nishirikalisilokuwa la kiserikalilinalofanyashughulizakekwakushilikiananaWizarayaAfyakatikaprogrammumbalimbaliambazoni;-

·         MapambanodhidiyaUkimwinaVirusivyaukimwi.

·         Uzaziwampango.

·         Kuzuiamagonjwayatumbonakuhara.

·         Mapambanodhidiya Malaria.

Kupitiaprogrammuhizo shirika linafanyakazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na vitengo mbalimbali katikaWizara vinavyo husika na programmu hizo.Kutokananaprogrammuhizoshirikalinafanyashughulizakekatikakuhakikishamagonjwahayoyanakuwahistoriakatikakila kaya naTaifakwaujumla,katikakufanyahivyobasihuwatunafanyashughulizifuatazo:-

·         Kutoaelimukwanjiayasinemajuuyaprogrammuzaafyatunazofanyiakazi.

·         Kubandikamabangoyenyeujumbezakupiga vita magonjwahayo.

·         Kutoaelimukwenyemabaakuhusuukimwinamatumizisahihiyakondomu (Bar promotions/Salama Nights).

·         Mauzoyabidhaambalimabalizaafyamfano:-

1.       Vifaakingadhidiyaukimwi mf Salamakondomu

2.       Bidhaazauzaziwampango

3.       Dawazakuuavijidudukatikamaji (Waterguards)



MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI:-

Katikamapambanodhidiyaukimwi Psi Tanzania kwakushirikiananaWizarayaAfyanawadauwengineinafanyashughulimbalimbalikatikakuhakikishakuwaugonjwahuuunatokomezwakabisakatikamkoawetunchiyetukwaujumla.Katikakuhakikishahilotunafanyayafuatayo:-

·         Kutoaelimukwajamiikupitiasinemaambazozinatoamafunzokatikakubadilishatabiazawatunamitizamoyaojuuyaugonjwahuu.

·         Kutoaelimukwenyemabaajuuyaugonjwahuupamojanaelimujuuyamatumizisahihiyakondomu.

·         Kuuza/Kuuzavifaakingakwaajiliyakujikinganaugonjwahuuyaanimipiraya kike nakiume.





i) Utoajiwaelimukwajamiikupitiasinema.

Psi Tanzania hufanyashugulizakezakuelimishajamiikwanjiambalimbaliikiwemonjiayakuoneshasinemaambazohutoaujumbejuuyanamnayakujikingaamakujiepushanaugonjwawaukimwi.Katikamwakahuukwamkoawamzimawa Tabora tumewezakuoneshasinemazenyeujumbejuuyaugonjwawaukimwikatikawilayazotezamkoanatakribanimaeneo 60 yavijijina kata mbalimbaliyamewezakufikiwanakuelimishwatokaJanuary mpakaNovembamwakahuu.

ii)Utoajiwaelimukwenyemabaa.

Shirika la Psi Tanzania piahufanyashughulizakuelimishawanajamiihasakwenyemabaawakiwemowatejanawahudumujuuyamatumizisahihiyakondomupamojaugonjwawaukimwi.

iii)Usambazajinauuzajiwavifaakinga.

Katikakutoahudumahiishirikauuzanakutoakwenyebaadhiyaasasimipiraya kike nakiumekwaajiliyakujikinganaugonjwawaukimwi.KwamwakahuumpakamweziNovembatumewezakusambazakiasi cha pakitizamipirayakiumemkoamzimakatikamgawanyoufuatao:-

·         Mipirayakiumepakiti 825,000zimetolewaburekwamakundimaalumuhasawaathirikakatikawilayazote

·         Mipirayakiumepakiti 1,533,600zimeuzwakwenyemadukayadawanavyakula

Psi Tanzania inatoashukranizadhatikwauhirikianomzuriinaoupatakutokaWizarayaafya ,wadaumbalimbalipamojanaofisiyaMgangamkuumkoa,wagangawakuuwawilayazote,piawakiwemowaratibuwaukimwiwawilayazotenawanajamiikwaujimla.

Tukumbukekwamba:-



“TANZANIA BILA YA MAAMBUKIZI MAPYA, UNYANYAPAA NA VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI INAWEZEKANA”



NB:Maadhimishoyasikuyaukimwikimkoayamefanyika kata yaUsisyawilayaniUrambomkoaniTabora,ambapomgenirasmialikuwamkuuwawilayayaUrambo.

Psi Tanzania kamamdauwamapambanodhidiyaukimwiilishirikikikamilifukufanikishasikuhiyo.