Wednesday, October 2, 2013

TAMASHA LA MUNDE STAR SEARCH LIMEGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MIL.TISA

 
Maelfu ya baadhi ya  wananchi mjini Tabora wakishuhudia fainali ya Tamasha la kuibua vipaji kwa wasanii mbalimbali lililojulikana kama MUNDE STAR SEARCH lililofanyika katika viwanja vya Stand ya zamani ya mabasi.
Mabondia wawili kutoka Camp mbalimbali za Boxers wa Tabora walipokutana jukwaani kwa ajili ya kutafuta ushindi katka mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Mh.Munde Tambwe ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa. 
Mdhamini mkuu wa Tamasha la Munde Star Search ambaye pia ni Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe akisalimiana na wapiga masumbwi wanawake wakati wa Tamasha hilo ambalo linatajwa kuwa litakuwa likifanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi mkoa wa Tabora.
 Wapiga masumbwi uzito wa juu katika Tamasha la Munde Star Search wakichuana vikali na kuonekana kuwa kivutio kikubwa katika Tamasha hilo lililogharimu zaidi ya shilingi Milioni tisa.
Wachezaji wa Karate ambao nao walipambana vikali katika Tamasha hilo kwa muda wa dakika sita

No comments:

Post a Comment