Wednesday, October 9, 2013

SERIKALI INATAMBUA FURSA ZA WALEMAVU WILAYANI UYUI MKOANI TABORA

MRATIBU WA WAJASILIAMALI NA HAKI ZA KAZI KWA WALEMAVU WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA HUSSEIN GEYA AKISOMA RISALA MBELE YA NKUU WA WILAYA YA UYUI LUCY MAYENGA

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALEMAVU MANISPAA YA TABORA JOHN KUKA AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA UYUI KWA AKIJI YA KUFUNGUA MAFUNZO

MKUU WA WIALAYA UYUI LUCY MAYENGA AKIFUNGUA MAFUNZO YA UJASILIAMALI NA HAKI YA KAZI KWA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA  UKUMBI WA KITUO CHA WANAFUNZI MJINI HAPA LEO

PICHA YA PAMOJA KATI YA MKUU WA WILAYA YA UYUI LUCY MAYENGA NA WATU MALI WENYE ULEMAVU MARA BAADA YA KUWAFUNGULIA MAFUNZO YA UJASILIA MALI NA HAKI YA KAZI KWA WATU WENYE ULEMAVU


NA LUCAS RAPHAEL TABORA




Halmashauri ya wilaya uyui mkoani Tabora kwa mwaka huu imetenga kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuwakopesha  vijana na wanawake ili kuweza kujiongezea kipato na kujiunga katika vikundi  .
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Uyui Lucy mayenga wakati akifungua mafunzi ujasiliamali na haki za kazi kwa walemavu iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha wananafunzi mjini hapa .
Alisema kwamba fedha hizo zitolewa katika makundi hayo ambapo vijana wametengewa kiasi cha shilingi milioni 20 na wanawake wametengewa kiasi kama hicho.
Alisema kwamba fedha hizo ukopeshwa kwa riba nafuu ili kuwawezesha vijana na kinamama  kufanya marejesho bila maumivu  .
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka walemavu hao kujiunga katika vikundi ambavyo vimesajiliwa na kuandaa andiko sanjari na kuwa na wathamini.
Awali mratibu wa mafunzo hayo Hussein Geya alisema kwamba mafunzo hayo yanalengo la kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu kupitia vikundi vya wajasiliamali vya watu wenye ulemavu kutoka katika wilaya hiyo ya uyui vilivyowezeshwa kikamilifu na kutambulika kisheria.
Alisema kwamba katika kipindi cha utekelezaji mradi huo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kutoa elimu kwa ajia ya redio na televishini ,kuendesha mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali kwa watu wenye ulemavu .

 Mafunzo hayo yameandaliwa na chama cha walemavu wilaya ya uyui mkoani Tabora na kufadhiliwa na shirika la Akiba Uhaki Foundation la nchini kenya




No comments:

Post a Comment