Wednesday, March 5, 2014

MTOTO WA MIAKA MITANO ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI,MAMA ACHOMWA MOTO KIFUANI-TABORA


Mwasiti Juma(21) akiwa na familia yake yenye watoto watatu hivi sasa amepata hifadhi katika Kambi ya kulelea watu wasiojiweza ya kijiji cha Amani manispaa ya Tabora baada ya kukumbwa na mkasa wa kufanyiwa ukatili wa kuchomwa moto kifuani na Mumewe anayefahamika kwa jina la Hamisi Kajuguja tukio ambalo lilitokana na mwanamke huyo kumkea mumewe wakati alipomkuta akimbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano ambaye pichani amevaa t.shirt nyeupe pembeni ya mama yake.
Mwasiti  ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nzubuka manispaa ya Tabora ameuambia mtandao huu kuwa mumewe amekuwa akimfanyia matukio mbalimbali ya ukatili kwa muda mrefu sasa na amekuwa akijaribu kuachana naye mara kadhaa lakini inashindikana,Matukio ya vitisho vya kuuawa yanayokwenda sambamba na vipigo imekuwa ni hali ya kawaida lakini jambo baya zaidi linaloendelea kumhuzunisha ni pamoja na hilo la kumbaka mtoto huyo ambalo limedumu kwa muda wa miaka miwili sasa.
Mtoto huyu  mwenye umri wa miaka mitano ndiye amekuwa akibakwa na baba yake kwa muda wote huo.Akielezea kwa undani zaidi kuhusu tukio hilo la ubakaji mama wa mtoto huyu Bi.Mwasiti Juma alisema mumewe kila siku ifikapo majira ya saa kumi na mbili asubuhi alikuwa akimuamsha na kumuaru kwenda kuchota maji kisimani huku yeye mwanaume huyo Hamisi Kajuguja akibakia na watoto nyumbani ambapo hupata fursa ya kufanya mchezo huo mchafu jambo ambalo pia linathibitishwa na mtoto mwingine huyo mwenye t.shirt   nyekundu kwenye picha ya juu kabisa....Hata hivyo Mwasiti baada ya kuchoshwa na matukio hayo ya mumewe aliamua kukimbia na watoto wake hao watatu hadi Tabora mjini mahali ambako alipata msaada wa kisheria ikiwa ni pamoja na kufika kituo kikubwa cha Polisi Tabora kuripoti adha hiyo hatimaye zoezi la kukamatwa kwa mumewe lilifanikiwa huku yeye Mwasiti pamoja na familia yake akipatiwa hifadhi ya muda kijiji cha kulelea watu wasiojiweza cha Amani.


No comments:

Post a Comment