Monday, August 25, 2014

FPCT YAPATA KANISA LA 18 KILOLENI TABORA

MAKAMU ASKOFU MKUU WA KANISA LA FPCT WILSON LAZARO WAKATI AKIZUNDUA UFUNGUZI WA KANISA HILO KILOLENI TABORA MJINI JANA

AKIKATA UTEPE KUHASHIRIA KUFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO LA FPCT

MTOTO FARAJA MUSA MWANAFUNZI WA SHULE YA AWALI KILOLENI AKISHEREHESHA UFUNGUZI WA KANISA HILO


WAUMINI WA KANISA HILO WAKIWA KATIKA MISA MAALUMU KWA AJILI YA UFUNGUZI RASMI WA KANISA HILO



Na Lucas Raphael,Tabora

KANISA la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT) limelaani vikali vitendo vionavyofanywa na baadhi ya watu kuwakata mikono walemavu wa ngozi Albino kwa imani za kishirikina.

Kauli hiyo ilitolewa  na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Wilson Lazaro kwenye sherehe za uzinduzi wa Kanisa la FPCT Palishi ya Kiloleni mjini Tabora.

Akizungumza katika uzinduzi huo Askofu Lazaro alisema vitendo vinaendelea kufanywa na watu kuamua kukata mikono ya mlemavu kwa tama ya kupata utajili wa haraka havina budi kulaaniwa na watu wote.

Askofu Lazaro aliiomba Serikali kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwanyima dhamana watu wanaofikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, lengo nikudhibiti matukio kama hayo yasiendelee kutokea katika jamii.

“Wewe kama huna fedha za kuendesha maisha yako hapa duniani nenda shamba ukalime sio kuamua kumkata mwenzako mikono eti tu umedanganywa na mganga wako wa kienyeji” alisema Askofu Lazaro

Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, Askofu huyo aliwaomba watanzania kuliombea kwa Mungu bunge la kutunga katiba, ili liweze kutunga katiba ambayo  itaweza kukidhi mahitaji, majawabu na matarajio ya watanzania wote.

Aliwataka wajumbe wa bunge la katiba kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi ya vyama vyao ili waeze kujadili kifungu kwa kifungu, ukurasa kwa ukurasa na hatimaye siku ya mwisho waweze kuwaletea watanzania katiba bora inayolenga kuinua uchumi wa kila mtanzania.

Katika sherehe hizo za uzinduzi wa kanisa hilo, pia uliambatana shughuli za kusimikwa kwa mchungaji kiongozi wa Kanisa la FPCT Kiloleni Peter Shani ambaye ndiye atakuwa mchungaji mkuu wa kanisa la mahali pale.

Mwisho




No comments:

Post a Comment