Wednesday, May 8, 2013

WIALYA ZA URAMBO NA KALIUA KUKUMBWA NA BAA LA NJAA .



NA LUCAS RAPHAEL,URAMBO 

 
Wakazi wa wilaya za Urambo na Kaliua watakumbwa na baa la njaa iwapo serikali na wananchi wenyewe hawata siamamia ipasavyo utunzaji wa chakula walichovuna  kutokana na mvua kuharibu vibaya asilima  35 za hekta ya zao la mahindi  yaliyolimwa msimu huu.   Akijibu hoja za madiwani kuhusu hali ya chakula katika wilaya hizo afisa kilimo  Erasto Konga alisema kuwa  uzalishaji wa mazao ya chakula msimu huu hasa mahindi siyo mzuri kutokana na kuharibiwa na ukame  kutokana na kutonyesha mvua wakati wa mwezi   wa pili na watatu.   Konga amebainisha kuwa makadirio ya chakula kwa wakazi  564,895 wa wilaya hizo mbili ni tani 195,776  hivyo  akatoa  wito kwa madiwani hao  kuwaelekeza wananchi  kununua chakula  hasa mahindi  kutoka maeneo mengine hapa nchini.   Aliongeza kuwa zaidi ya tani 90,000 za chakula kinachozalishwa na wakulima wa wilaya hizo ni  cha wanga huku wananchi wakipendelea kutumia  kwa wingi mahindi  kama chakula   japo wananalima  mpunga ambao ufanywa kama zao la biashara.   Afisa kilimo huyo ameliambia gazeti hili kuwa kiashiria moja wapo ambacho  kinaonyesha kuwepo kwa tatizo la njaa ni kutokana na kutoshuka kwa bei ya mahindi hadi sasa kwani debe la mahindi kung’ang’ania  shilingi 9000/= badala ya thsh 3500/= au 4000/= wakati wa msimu wa mavuno hali ambayo inaonyesha kwamba mahindi hayapo.   Konga ameongeza kwamba bado wimbi la walanguzi linatishia hali ya chakula katika wilaya hizi mbili  kwani pamoja na serikali kuwahimiza wananchi wasiuze chakula lakini wengi wao ulazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kujipatia mahitaji.   Amesema kuwa uzalishaji wa zao la muogo pia utapungua msimu huu kutokana na zao hilo kukumbwa na ugonjwa wa BATO BATO KALI  hivyo kuongeza .   Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2012 / 2013 zilipangwa kulimwa hekta 
135, 704 za mazao ya  chakula  ambazo zilitarajia kuzalisha tani 325,465
ambapo hekta za mazao ya chakula zilizolimwa ni 131, 785 sawa na asilimia
 97 ya lengo.

 

Naye mkuu wa wilaya hiyo Anna  Magowa aliwataka watendaji kutafuta ni 
jinsi gani watakabiliana na tatizo hilo la upungufu wa chakula hasa mahindi 
ambao umekuwa ukiikumba wilaya hiyo mara kwa mara.

 

Aliongeza kuwa watafute uwezekano wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji
hasa utumiaji wa matone kwani ndio hatumii maji mengi kwenye mazao ya 
mahindi  kutokana na tatizo la upungufu wa mvua.

 

MWISHO.

No comments:

Post a Comment