Monday, May 13, 2013

WAANDISHI WA HABARI WAPO HATARINI - TUNDU LISSU


lisu1 fda6e
Mh Tundulisu akitoa Vyeti kwa wana chaso katika Haflahio,

WAANDISHI wa habari wapo katika hatari kubwa ya kutoweka nchini kutokana na kuandika maovu yanayofanywa na viongozi wa serikali.
Haya yamezungumzwa na Mbunge wa Singida Mashariki na mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu katika mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa (CHASO) katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kilichopo katika Manispaa ya Iringa.
Lissu alisema waandishi wa habari wapo katika hatari ya kutoweka hasa kwa kuuawa kutokana na ukweli wao wanaouandika hasa kuyaweka madudu ya baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema hasa katika ripoti ya uchunguzi ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ya tume iliyoundwa na vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) inaonesha wazi juu ya hatari walionayo waandishi wa habari.

Alitaja chanzo cha kuwamaliza waandishi hao kuwa ni polisi wanaotumiwa na viongozi hao kama njia ya kuzuia kuendelea kuandika madudu yao.
Hata hivyo alisema waajiri wa waandishi ni chanzo moja wapo cha kinachochangia waandishi kuwa katika hatari hiyo kwa kuwatengenezea mazingira mabovu ya utendaji wao hasa wawapo kazini.
Lissu alisema waandishi wa habari ambao wapo katika hatari kubwa ni wa Iringa ambao tayari wapo katika listi ya kupotezwa kwa namna yoyote kwa kile kilichoelezwa kuwa hawaandiki habari zao kwa unafiki.
"Tuwalinde sana waandishi wa habari kwa kweli wapo katika hatali kubwa sana. Kila mmoja awe mlinzi wa waandishi hawa na ifike mahali tukasema hatutaki Mwangosi mwingine. Hasa waandishi hawa wa Iringa wapo katika wakati mgumu sana" alisema.
Pia aliwaasa wanafunzi waliomaliza kwenda kuungana na wananchi kuendeleza harakati za Mageuzi kuanzia katika Mashina,kata, na Majimbo ili kufanikisha mpango wa kuelekea ikulu vinginevyo ni ndoto hapondipo utatokea ukombozi wa Waalimu, Madaktari, na Wanasheria
Wasio na kazi kwasababu ya Mipango mibovu ya utawala uliopo kupata furusa ya kuitumikia nchihii kukiandaliwa mipango mizuri ya ajira,
Historia inaonyesha hakuna Mzee aliefanikisha mapinduzi ya kisiasa katika nchiyake kama hakuanza wakati akiwa kijana na kuelekea katika Mafanikio ndipo uzee unamkuta akiwemo ndani ya Harakati,

No comments:

Post a Comment