Friday, July 18, 2014

WASIO NA KADI YA BVR KUTOPIGAKURA 2015-KIGOMA,TUME



Na Magreth Magosso,Kigoma


IMEELEZWA kuwa,wananchi wasiokuwa na vitambulisho vya mfumo wa Biomertic Voter Registration hawatahusika katika mchakato wa kupiga kura wa maoni  na uchaguzi mkuu 2015.


Akifafanua hilo Kamishana wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Hamid Mahmoud  alisema  wanananchi hawana budi kupokea mfumo huo,ambao ni tiba ya kuondoa changamoto ya uchakachuaji wa mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara mbili.


“huu mfumo wa BVR inachukua taarifa za kibailojia ya muhusika hivyo si rahisi kuibika inatambua tabia,alama za vidole,sura,mpangilio wa mikono,mboni ya jicho,sauti  na harufu ya mtu na kuhifadhiwa katika kanzi data na  jamii ishiriki  kujiandikisha.” A libainisha Mahmoud.


Alisema mchakato upo kwa watu wote, walio na kadi ya kupigia kura za awali zenye mfumo wa `optical mark recognition’  kutoa picha papo kwa papo na wale ambao wanatarajia kutimiza miaka 18 ifikapo 2015 wanawajibika kushiriki  kupata kadi ya `BVR’ ili kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura.


Kwa  upande  makam Mwenyekiti wa tume  ya Uchaguzi Taifa Mohamed  Kiboko alibainisha changamoto za awali ni pamoja na kushindwa kubadilisha taarifa za mtu kwa wakati husika,majina kujirudia zaidi ya mara moja,kuwepo na majina ya marehemu na kutoonekana kwa majina ya wapigakura.


Alisema  wananchi walio na kadi za awali wanahitajika waende na vitambulisho hivyo ili wapewe vitambulisho vya kisasa na endapo atakuwa amehama au kubadilisha taarifa zake inabidi atoe taarifa husika kwa mwandishi mapema ili kurekebisha na kumwezesha kupiga kura eneo husika.

Aliongeza kwa kusema wananchi wasio raia wa hapa watabainika kupitia wadau wao kama tasisi ya Rita na Nida katika kuthibitisha data za muhusika na kuomba wananchi wawe wazi kuwafichua wahamiaji wasio rasmi ili wasitumie fursa hiyo.


Aidha itambulike kuwa,taifa hili si ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo kutokana na nchi kadhaa wanatumia mfumo wa BVR ikiwemo Zanzibar(2009),mali(2005),Nigeri(2007)Ghana(2009),Uganda(2008),Kenya(2013),Liberia(2005),Zambia(2008),Afrika kusini (2009),guinea(2005.


Alisema changamoto zilizojitokea katika mataifa hayo hayahusiani na mfumo huo wa Biometric na kudai mfumo huo ni tiba sahihi ya changamoto za awali ambazo ziliikwaza tume hiyo na serikali husika.

No comments:

Post a Comment