Wednesday, October 22, 2014

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF WASHIRIKI WIKI YA VIJANA KITAIFA TABORA

Meneja mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kanda Bw.Emmanuel Adina akijaribu kutoa maelezo kuhusu mfuko wa afya ya jamii CHF na tiba kwa kadi maarufu TIKA kwa mmoja kati ya wananchi waliotembelea Banda la maonesho la NHIF wakati wa wiki ya vijana kitaifa mkoani Tabora.
Mmoja kati ya maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima Uzito na Urefu mmoja kati ya wananchi wa Tabora waliotembelea Banda la NHIF na kupima afya zao wakati wa wiki ya vijana  kitaifa mkoani Tabora.
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF Bi.Catherine Kameka akitoa maelezo kwa mwandishi wetu wakati alipotembelea Banda la Mfuko huo.
Baadhi ya wananchi walijitokeza kupima afya zao


Baadhi ya maafisa wa NHIF wakiendelea kufuatilia taarifa mbalimbali kwenye mtandao ambazo wanazitumia katika maonesho hayo kuielimisha jamii umuhimu wa kutunza afya zao.
Banda la Chama cha msalaba mwekundu
Mabanda mbalimbali ya maonesho katika wiki ya vijana kitaifa mkoani Tabora





No comments:

Post a Comment