Monday, February 2, 2015

KAMPUNI YA MURHANDZIWA YAKABIDHIWA LESENI YA KUENDESHA BAHATI NASIBU YA TAIFA

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Abbass Talimba (kushoto) akikabidhi leseni kwa VIongozi wa Kampuni ya Murhandziwa ambao ndio wamepewa kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa nchini Tanzania.Aliyeshika Leseni hiyo ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece.
Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton - Masaki.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa ambayo itakuwa ikiendesha bahati nasibu hiyo hapa nchini ambapo Bahati nasibu hiyo itaanza mnamo tarehe 4 Julai 2015.

Bei ya tiketi zitakazouzwa itagharimu shilingi za Kitanzania shilingi 150.

No comments:

Post a Comment