Thursday, February 5, 2015

POLISI TABORA WAFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI KIJANA MMOJA AKIWA NA RISASI 356 ZA SMG


Jumla ya risasi 356  za SMG zilizokamatwa askari Polisi  kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Wolfram Msemwa(32) huko katika mtaa wa Kazehill kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora.
Kitambulisho cha mtuhumiwa aliyekutwa na risasi hizo ambaye kabla ya kukamatwa tarehe 2/2/2015 aliwahi kuwakimbia askari Polisi  mnamo tarehe 23/11/2014 na kutelekeza begi alilokuwa amehifadhi bunduki aina ya SMG na risasi 17 katika eneo la Mazinge hospitali ya wilaya ya Sikonge

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akiwaonesha waandishi wa habari risasi zilizokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo Wolfram Msemwa anayedaiwa amekuwa na mtandao na baadhi ya waharifu kutoka nchi jirani na Tanzania kwa upande wa Magharibi.


1 comment:

  1. Safi Sana kikosi cha ulinzi tabora kwa kazi hii nzuri,shime wananchi kuwafichua wahalifu popote walipo Na vyovyote walivyo.nchi haitofikia maendeleo pasi Na amani Na usalama wa raia Na mali Zao.

    ReplyDelete