NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
IMEELEZWA KUWA Suala la
kijinsia halina budi kupokelewa ili kumpa nafasi mwanamke yakuweza kuchangia
maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla .
Kauli hiyo ilitolewa na mmoja
ya wakazi wa kijiji cha Kigwa AZIZA RAMADHANI wakati akichangia mdahalo wa Mwanaume
na mwanamke.
Kauli hiyo, waliitoa jana
kijijini hapo kwenye mdahalo wa usawa wa kijinsia na maendeleo,
ulioandaliwa na Shirika la mtandao wa mandeleo ya jamii wilayani Uyui (UCODEN)
kwa ufadhiri wa The Foundation for Civil Society kutoka Dar es Slaam.
Alisema kwamba mwanaume na
wananmke washauriane katika shughuli mbalimbali ili kujiletea maendeleo.
“Mwanaume asijione kuwa
yeye ndiyo binadamu na mwanamke ni mashine ya kufanya kazi katika jamii.”alisema
AZIZA
Alisema kwamba kila mtu ana sehemu yake katika kuleta
maendeleo katika jamii.Tatizo ni kina baba kujiona kuwa wapo juu kuliko
mwanamke bila kujali uwezo alio nao mwanamke.
Alisema kuwa baba pekee yake hawezi
kuleta maendeleo ni lazima kuwepo na mchango wa mwanamke.
Amina Christopher Mjema:naye alisema kuwa wazazi wengi wananchangia mtoto wa kike kushindwa kufanya
vizuri katika elimu kutokana na tabia ya wazazi kuhamasisha watoto wao wa kike
kuolewa badala ya kuhamasisha watoto hao kusoma zaidi.
Hata hivyo Diwani wa kata
ya Kigwa Katyavi Salumu alisema kwamba kuna na changamoto nyingi katika masuala ya
kijinsia mfano kipigo kwa kina mama limekuwa tatazi kubwa kwa jamii yetu.
Alisema kwamba mgawanyo
hafifu wa mali,hii inatokana na kurithi tabia kutoka kwa mababu bila kuangalia
athari za mila hizo za mababu.
Aliongeza kusema kwamba pia
kina mama wanajirudisha nyuma kutokana na kushindwa kwao kutoa maamuzi ya jambo
fulani na badala yake wamekuwa wakiwasubiri waume zao.
Kwa upande wa elimu, diwani
huyo alisema watoto wa kike nao wamekuwa wakichangia katika kuwanyima fursa ya
elimu kutokana na mabadiliko ya ukuaji ni vema jamii kuangalia kwa makini
kuhusu malezi ya vijana.
Hata hivyo Mratibu wa UCODEN
Christopher Nyamwanji aliwashukuru sana washiriki kwa maoni yao ambayo
yameonesha uzoefu wa masuala ya kijinsia katika kata ya Kigwa na pia aliwasihi
wakazi wa Kigwa kujitokeza tena siku nyingine katika shughuli kama hii.
MWISHO