Monday, June 17, 2013

"MARUFUKU KUWATUMIKISHA WATOTO KWENYE MASHAMBA YA TUMBAKU"-SERIKALI KALIUA


Baadhi ya watoto wa Shule ya msingi Igwisi ilyopo kijiji cha Igwisi wilayani Kaliua mkoani Tabora wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga ajira mbaya kwa watoto.
Hawa ni miongoni mwa watoto ambao hawajapata fursa ya kupata elimu ya msingi ambao wanaishi katika kijiji cha Igwisi wilayani Kaliua.
Mkurugenzi mtendaji wa Mradi wa Prosper Bi.Mary Kibogoya akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kuzuia  na kuwaondoa watoto wapatao 7,800 kwenye utumikishwaji katika mashamba ya tumbaku.
Watoto katika maadhimisho hayo waliimba nyimbo zilizohamasisha jamii kupambana na tatizo la ajira mbaya kwa watoto kwenye mashamba ya tumbaku.
Wakati wa maadhimisho hayo ngoma ya asili ya wenyeji wa Mkoa wa Rukwa ilitumbuizwa na baadhi ya kinamama na kusababisha maafisa wa Mradi wa Prosper na makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao la tumbaku kuanza kucheza na kuwa kivutio kikubwa katika maadhimisho hayo.
Afisa tarafa ya Kaliua Bw.Josephat Brown ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kaliua katika maadhimisho hayo ambapo Serikali ilitoa tamko la kumchukulia hatua kali yeyote atakaye jihusisha na utumikishwaji wa watoto na kusababisha watoto kukosa fursa ya haki ya elimu.






No comments:

Post a Comment