Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana jioni mjini Dodoma.
Tukio hilo lilitokea jana jioni wakati Mh. Machalli
akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya
kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara
ili wasogee pembeni naye aweze kupita ....
Kitendo hicho kilionekana
kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa
nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli
kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni ....
Baada ya kushuka, vijana
hao walimtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa
hasira ndipo kipigo kikali kilipoanza.
Shuhuda aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Shuhuda aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.
No comments:
Post a Comment