Mkutano wa kwanza wa wadau wa CG FM
Radio unaendelea katika ukumbi wa Kalindimya -Moravian hostel Tabora
ukiwa na lengo la kujadili juu ya uanzishwaji wa vipindi vipya vya
kijamii vya Nufaika na Fumbuka.Vipindi hivi vya kijamii vinatarajiwa
kuanza kurushwa hivi karibuni kupitia CG FM Radio.Mkutano umehudhuriwa
na wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia,vyama vya ushirika na
makampuni mbalimbali
MKURUGENZI WA 89.5 CG FM RADIO BW.CHARSE GEORGE
MENEJA WA 89.5 CG FM RADIOBW. TITUS PHILIPOSAMADA
MADUHU | MSHAURI WA VIPINDI KATIKA KITUO CHA MATANGAZO CHA 89.5 CG FM
RADIO CHA MKOANI TABORA AKITO MAWASILISHOYAKEYALIYOTOA MWONGOZO WA NINI
KIMEWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI MKOANI HAPO TABORA
WADAU WAALIKWAWADAU WAALIKWA
wazee wa mitambo
Meneja wa mamlaka ya haliya hewa Tabora na Mpanda
Wadau wakisikiliza kwa umakini
Meneja wa mamlaka ya hali ya hewa akitumia mchoro kuelezea hoja
Ibrahim Haruna-Mtangazaji na muandaaji wa kipindi cha FUMBUKA | Akikitambulisha kipindi hicho kipya.
(PICHA NA Aloy-Son-Blog)
-------------------------------
CG FM RADIO IMEKWISHA ONESHA KIPINDI
KIPYA CHA NUFAIKA KITAKACHOLENGA KUJIHUSISHA NA MAMBO YA WAKULIMA KWA
KUWAPA ELIMU, UTOAJI TAARIFA ZA HALI ZA HEWA, KUSHIRIKISHA WATAALAMU NA
WADAU WAKIWEMO WAKULIMA WENYEWE KUJADILI MAMBO YAHUSUYO KILIMO KWA
MANUFAA, TAARIFA ZAAIDI ZITATOLEWA KUHUSU BEI NA MASOKO, TAARIFA ZA
TAFITI ZA KILIMO.
-----------------------------------------------------------------
MAWASILISHO YA WADAU
====================================
MKUU WA CHUO CHA KILIMO CHA TUMBI
- Aina mpya ya mpunga iitwayo AMKA/NERICA- Mradi wa Wajapani
- Kilimo SHADIDI (Mazao maradufu
MRATIBU WA KILIMO MIRADI VIIJIJI VYA MILENIA-MBOLA
- Kanuni bora za kilimo
- Matumizi sahihi ya mbolea
- Ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya kilimo
- Mikopo naafuu kwa mkulima
- Usisitizaji wa mbegu stahimilifu za maeneo ya Tabora.
MENEJA WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TABORA NA MPANDA.
- Upimwaji wa hali ya hewa na uwasilishaji wake kwa jamii kupitia vyombo vya habari
- Matumizi ya hali ya hewa kwenye kilimo, usafirishaji, maji, nguvu za uzalishaji, utalii.
- Utoaji wa taarifa za hali za hewa kwa misimu (siku 10 na kuendelea)
- Umuhimu wa hali ya hewa kwa kilimo (utambuzi wa udongo n.k)
- Madhara ya hali ya hewa- ukame, migogoro ya wafugaji na wakulima, ugomvi wa maji, mafuriko,n.k
MUWAKILISHI WA CHUO CHA ARDHI
- Umuhimu wa sheria za usimamizi na matumizi bora ya aridhi
- Kujua taratibu za kisheria ya aridhi zilivyo na mamlaka zake
- Mpango wa matumizi bora ya aridhi na faida zake.
- Hati za haki miliki za aridhikama zakimila na nyinginezo.
- Umuhimu wa nyuki kiuchumi na kibaolojia.
- Teknolojia ya ufugaji nyuki na tafiti.
- Ubora wa asali na mabadiliko ya mbinu zaufugaji nyuki kupitia teknonojia.
- Mbinu bora za kisasa katika uvunaji asali (Teknolojia Mwafaka).
- Zana na aina zake za uvunaji asali (Gun-boot, Kofia,groves n.k)
- Faida za ufugaji nyuk
- Umuhimu wa mimea kwa nyuki
MAWASILISHO YA WADAU YALIKUWA YAKILENGA
UPATIKANAJI WA NAMNA UBORESHWAJI WA VIPINDI VIPYA VIMLENGAVYO HASA
MKULIMA WOTE NA WAFUGAJI KWA KUTOA MWANGA NA MWELEKEO HATA PIA KATIKA
KUSHIRIKIANA KUIKOMBOA JAMII YA WANATABORA KWA WAO KUUONA UMUHIMU WA
KITUO CHA RADIO KWA MANUFAA YAO.
No comments:
Post a Comment