Na
Lucas Raphael,Tabora
JUMLA
ya malalamiko 36 yalipokelewa na ofisi ya maadili kanda ya
magharibi katika kapindi cha mwanka jana na mwaka huu kwa maafisa wa mahakama
kwa kuchelewesha kesi na kupokea rushwa kwa lengo la kupendelea hukumu.
Maelezo
hayo yalitolewa na kamishna wa sekretarieti ya maadili ya viongozi jaji
mstahafu Salome Kaganda alipokuwa akimkaribisha mkuu wa mkoa wa tabora Fatma
Mwassa wakati wa kufungua mafunzo kwa mahakimu katika ukumbi wa mtemi
Isike mwanakiyungi mkoani tabora jana .
Alisema
kwamba katika malalamiko hayo 15 sawa na asilimia 41 .6 ni malalamiko kwa
maafisa wa mahakama ,wakiwepo majaji na mahakimu wa ngazi mbalimbali kwa
kuchelewesha kesi na kupokea rushwa .
Jaji
Kaganda aliendelea kusema kwamba idara ya mahamaka ni miongoni mwa Idara
za serikali zinazolalamikiwa sana kwa vitendo vya Rushwa ,kutokutenda haki na
kukosekana kwa uadilifu.
Alisema
kwamba mafunzo hayo lengo lake ni kuwajengea uwezo viongozi wa katika kuifahamu
na kuitekeleza sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995
ambayo ndio sheria mama inayosimamia maadili ya viongozi wa umma nchini.
Hata
hivyo mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwassa akifungua mafunzo hayo katika hotuba
yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Sulemani Kumchaya alisema kwamba
utumishi wa umma kwa ujumla bado una matataizo na mapungufu mengi ya kimaadili
,utoaji wa huduma usioridhisha ,migongano ya maslahi matumizi mbaya ya madaraka
hivyo vyote ni changamoto inayowakabilia watumishi walio wengi hapa nchini .
Alisema
kwamba mafunzo haya yawe ni chachu ya mabadiliko kwa kada ya mahakimu mkoai
hapa kwa kufanya kazi kwa kufuata maadili kanuni sheria na busara .
“hali
hiiitakuza matumaini na imani ya wananchi kwa serikali na hususani mhimili wa
mahakama kama chombo kikuu cha kusimamia haki kwa umma”alisema mwassa.
Mafunzo
hayo yaklioandaliwa na ofisi ya maadili ya viongozi kwa mahakimu kwa
wafawidhimkoa na wilaya na wale wa mahakama za mwanzo kutoka katika wilaya saba
za mkoa wa tabora .
Mwisho
No comments:
Post a Comment