Vurugu
tupu: Ofisa wa usalama na watu wengine wakijaribu kumbeba askari wa
kike aliyepata majeruhi katika mapokezi hayo yaliyojaza nyomi kubwa sana
Kabla ya fujo: Maelfu ya watu wamejitokeza kumpokea nyoa Beckham katika chuo kikuu cha Shanghai
Maskini askari: Askari wa kiume akiwa amelala chini ya sakafu baada ya kujeruhiwa katika mapokezi hayo
Fujo zaanza: Maofisa wa polisi wameshindwa kuwazuia maelfu ya watu katika mapokezi hayoNa Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nyota
wa zamani wa Manchester United, Los Angel Galaxy, Real Madrid, PSG na
timu ya taifa ya England, David Beckham amewasili leo nchini China na
kusababisha wanafunzi watano kujeruhiwa vibaya katika harakati za
kumpokea katika chuo cha Tongji University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
Beckham
ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira wa miguu ya chuo hicho
kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye lengo la
kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha
ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono na nyota huyo,
imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha watu
kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo
la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa kutimia kufuaia fujo
hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika mtandao wake wa
kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile
kilichotokea.
Samahani
sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo kikuu pale uwanjani,
kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia watu wachache
wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri wapone
salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani
watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo na kuhitaji kumshika
nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa maofisa wake
watu wamejeruhiwa katika fujo zoezi hilo.
Beckham
mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka msimu uliopita ambapo
aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, Ligue 1.
No comments:
Post a Comment