NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Serikali imewataka
wakulima wa Tumbaku mkoani Tabora kuacha kutorosha Tumbaku nje ya mkoa huo na
kuiuza katika masoko maalum ya maeneo yaokwani hawatakwatwa fedha zao kwa mwaka
huu na mabenki yanayovidai vyama vya msingi.
Mkuu wa mkoa wa
Tabora ,Fatuma Mwassa, ametoa kauli hiyo alipokwenda kutembelea maghala ya
kuhifadhia Tumbaku eneo la Kiloleni mjini Tabora, ikiwa ni kuwatoa hofu
wakulima wa zao hilo wanaohofia kukatwa fedha nyingi na taasisi za fedha.
Alisema mgogoro baina
ya taasisi za fedha na vyama vya msingi vya wakulima wa Tumbaku hautawahusu
wakulima hao kwa sasa wapeleke zao hilo katika masoko yao kwa kupitia vyama
vyao vya msingi.
Akifafanua
mkuu wa mkoa amesema kwamba serikali imweka utaratibu utakaowezesha taasisi za
fedha na vyama vya msingi kuzungumza na kufikia muafaka bila ya kuwakata wakulima
fedha zao halali zinazotokana na malipo ya Tumbaku.
Mwassa,
aliwataka wakulima wa Tumbaku kutohofu kuuza Tumbaku katika masoko maalum
yaliyopangwa na kuacha kutorosha Tumbaku na kuiuza nje ya mkoa huo.
Alisema
hivi karibuni baadhi ya wakulima wa Tumbaku katika wilaya za mkoa wa Tabora
wameanza kutorosha Tumbaku nje ya mkoa huo kwa kuhofia kuhusishwa na makato
yanayotokana mgogoro wa madeni baina ya taasisi za fedha na vyama vya msingi
vinavyowawakilisha katika mauzo na mikopo ya pembejeo.
Jambo hilo
limepelekea wa kulima wengi kushindwa kupeleka Tumbaku yao sokoni hadi hapo
hali itakapotengemaa na hivyo kuleta sinto fahamu ya biashara ya zao hilo mwaka
huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment