NA LUCAS RAPAHEL,TABORA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma akiangalia magunia ya bangi yaliyokamata Wilayani Nzega ambayo yalikuwa yakisafirishwa,mzigo huu ulikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi mil.68. |
JESHI
la Polis wilayani Nzega mkoani Tabora linawashikilia watu wa 4nne kwa tuhuma za
kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya bangi zaidi ya gunia sita 6sawa la kilo
168 zikisafirishwa kuelekea mkoani Shinyanga zikiiwa na thamani ya shilingi
milioni 68.7.
Akizungumza
na waandishi wa Habari kamanda wa polis mkoani Tabora Peter Ouma alisema kuwa
Tukio hilo limetokea June 6 mwaka huu katika kijiji cha kilabili kata ya
Nata wilayani hapa majira ya saa tatu asubuhi.
Alisema
kuwa Jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu
wanapitisha madawa hayo aina ya bangi.
Alisema
kuwa kwa kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi wema Jeshi hilo liliweka mtego
mkari ambapo ulifanikisha kuwa nasa wahari hao wakiwa na madawa hayo aina ya
bangi magunia sita (6).
Alisema
kuwa wahalifu hao wakiwa wamebeba bangi hizo kwenye baiskeli kila mmoja magunia
mawili mawili wakitokea kijiji cha ugembe nzega kuelekea Manonga tinde mkoani
shinyanga.
Kamanda
Ouma aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Paul Batoni (41)mkazi wa
manonga tinde shinyanga,Kashindye Seleli(21) mkazi wa manonga Tinde
shinyanga,Shaya kapaya(20)mkazi wa manonga tinde shinyanga pamoja na Moshi
Joseph (22)mkazi wa Ugembe puge shinyanga.
Alisema
kuwa Jeshi la polis linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa mahojiano zaidi
ilikupata mtandao huo wa usambazaji wa madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na
kuongeza kuwa pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahamani kujibu
tuhuma hizo zitakazo wakabili.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment