Monday, June 17, 2013

WAZIRI MKUU AWAONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUMZIKA MZEE TIMOTH APIYO


 


Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Timoth Apiyo likiwazili Makaburini kwa kubebwa na Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jeneza likiingizwa kaburini.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiweka udongo kaburini.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiweka shada la maua kaburini.

Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Mke wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa msiba huo.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda,ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Marehemu Timoth Apiyo,yaliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Marasibora mkoani Mara.

Waziri Pinda alitoa pole kwa familia na wakazi wa Kijiji cha Mara Sibora,Wilaya ya Rorya na Mkoa wa Mara kwa kumpoteza kiongozi na mzalendo aliyeitumikia nchi yake kwa uadilifu.

Wengine waliohudhuria maziko hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu),William Lukuvi;Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue; Makatibu Mkuu Viongozi wastaafu, Balozi Paul Rupia, Balozi Marten Lumbanga na Philemon Luhanjo pamoja na mke wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere.

No comments:

Post a Comment