Mkuu wa wilaya ya sikonge mkoni
Tabora Hanifa Selengu amewataka watumishi wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa
kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuepuka matatizo yanayoweza
kuwapata kwa kukwepa kutozifuata sheria hizo .
wito huo aliutoa wakati akizungumza na
watumishi wa wilaya hiyo kwa mara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa na Rais
kushika wadhifa huo katika wilaya hiyo.
Aliwataka watumishi wote wafanye kazi kwa
ushirikiano ,ikiwa ni pamoja na kushirikiana na madiwani katika shughuli zote
za maendeleo katika kata zao kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini.
Hanifa amewataka watendaji wa vijiji na
kata kuwahimiza wananchi katika sehemu zao kujumuika kwenye usafi wa mazingira
ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuwapata wananchi bila ya wao kutambua.
Alisema kuwa kila jumamosi iwe siku ya
usafi katika wilaya ya sikonge ikiwa ni usafi wa vyoo ,mazingira yanayozunguka
maeneo ya biashara ,nyumba na mifereji ,ambapo sheria ndogo zitatumika kwa
ajili ya kuchukulia hatua watu wakaokaidi .
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wakuu
wa idara nawatendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya ya sikonge na
watumishi wa chini yao kufanyakazi kama timuya ushindi kwa kufuata sheria
kama zilivyowekwa na serikali za mitaa .
Hanifa alendelea kusistiza watumishi
kufanya kazi kwa bidii,kujituma na kutoa mrejesho wa shughuli zao na kuwataka
kuwahamasihsa wananchi wa wilaya hiyo ambapo kila kaya kuwa na mpango kazi wa
maendeleo .
Ametoa onyo kwa watendaji wanajifanya
kuwa mungu watu bali watumishi wote wa wilaya hiyo ni watumishi wa wananchi na
kuwaletea maendeleo.
Mwisho
WANAWAKE.
Vikundi vya wananwake katika halmashauri ya
wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wametakiwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili
kuweza kutimiza azima ya vikundi hivyo kuwaletea maendeleo wao ,familia zao na
taifa kwa ujumla.
Ushauri huo ulitolewa na mkurungezi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge ,Paul Nkulila katika halfa fupi ya
kutoa mikopo kwa vikundi vya kimama katika ukumbi wa halshauri huyo ambapo
vikundi 12 vyenye wananwake 120 walipatiwa kiasi cha shilingi milioni 12.
Alisema kwamba vikundi hivyo vya kinamama
vinapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa kipindi walichofunga mkataba ili
kuwezesha wananchi wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo kwa ajili ya kusukuma
maendeleo kwa wanawake .
Mkurungezi huyi wa halmashauri ya wilaya ya
sikonge amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuvitembelea vikundi hivyo mara
kwa mara na kuvishauri jinsi ya uzalishaji katika biashara zao .
Aidha Nkulila amewataka wananwake hao kuwa
na upendo miongoni mwao na wazidishe mshikamano na siyo kila mtu anafanya kazi
kivyake vyake upendo ni lazima ,kwanimkufanikiwa kwa mwanamke mmoja wao ni
mafanikoa makubwa kwa wanawake wote wa wilaya ya sikonge.
Awali akitoa taarifa kwa mkurungezi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya sikonge ,afisa maendeleo ya jamii,
Hemistocles Byarugaba alisema kwamba idara hiyo ya maendeleo ya jamii
imevitembelea vikundi mbalimbali ilivyoomba mikopo ili kudhibitisha kuwa
wanayo miradi waliyoombea mikopo na dida hiyo imefuatilia mara kwa mara
urejeshai wa mikopo kwa waliokopa katika vipindi tofauti.
Alisema kwamba ameitaja baadhi ya miradi
iliyoombea mikopo kuwa ni migahawa ,kilimo,biashara ,vioski na maduka .
Mingine ni vikundi vya ushonaji na wa
vyerehani,na biashara ndogo ndogo na kuongeza kuwa mikopo ya wanawake
imesaidaia sanan katika jamii kwa kuondoa migogoro midogo midogo ya
kifedha kwa familia .
MWISHO.
NZEGA WAISLAM.
KIKUNDI cha wanaharakati wa wakiislam
wilayani nzega mkoani Tabora kinatarajia kuwafungulia mashtaka viongozi wa
baraza la waislam tanzaznia wilaya ya hiyo (Bakwata} kwa ubadhifu wa fedha wa
zaidi ya shilingi billion 4.8
Fedha hizo ambazo kwa kipindi cha miaka
saba hawajawai kusomea taarifa ya mapato na matumizi na bazaar hilo la kiisilamu wa wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani
hapa,kiongozi wa kikundi hicho shekhe YUSUF SHABANI.alisema kwamba kwa kipindi
chote hicho cha miaka saba hawajui jinsi gani fedha hizo zilivyotumika kwa
kipindi cha miaka hiyo saba.
Alisema kwamba wameamua kuwapeleka viongozi
hao mahakamani kutoka na baadhi ya viongozi hao kuhujumu miradi ya waislam.
Shabani alisema kwamba fedha hizo
zilitokana na michango ya waislam waliochangia michango kwa ajili ya mahabara
ya shule ya sekondari ya BADRI kiasi cha shilingi milioni 645.1,ambapo mahabara
yenywe bado hajaisha na fedha hazijulikani zilipo.
Alisema licha ya michango ya shule lakini
ia fedha za zahanati ya bakwata ziadi ya shilingi bilioni 1.2 hazijulikani
zilipo fedha hizo na hazijulikani zilipo.
Kiongozi huyo wa kiislam taarifa ya
uendeshaji bwa miradi ambayo bakwata wanapata ni machinjio ya mjinbi
nzega,vibanda kuzunguka msikiti wa Ijumaa na ule wa majengo,mnada katika eneo
la nzega mjini .
Nyingine ni nyumba,majengo na viwanja vya
wakfu,sadaka za Ijumaa na mwezi wa ramadhani,na nyakati nyingine wanaamua
kufadhili kusaidia ,zahanati ya bakwata na shule ya sekondari ya badri.
Mwisho
No comments:
Post a Comment