Na Lucas Raphael,Tabora
CCM
Kinyanganyiro
cha kuwania nafasi ya wenyeviti wa mkoa na wilaya kimepamba moto baada ya
wananchma wa chama cha mapinduzi kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi wa chama hicho.
Waliojitokeza
kuchukua fomu hizo ni wale waliokuwa wakishikilia
nafasi zao za uongozi na wengine kujitokeza kwa mara ya kwanza kuwania uongozi
wa chama hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari katibu msaidizi wa mkoa wa Tabora ,Elia Kimaro alisema
kwamba hadi kufikia jana ni mwenyekiti anayemaliza muda wake Hassani Wakasuvi ndiye
alikuwa amechukua fomu kwa ajili ya kutetea kiti chake hicho.
Alisema
kwamba muda bado hupo hadi angasti 28 mwaka huu ambayo itakuwa ndio siku ya mwisho
kuchukua na kurudisha fomu hizo kwa nafasi ya mwenyekiti na wajumbe wa
halmashauri kuu ya Taifa (nec)
Katika
wilaya za Uyui waliojitokeza kuchukua fomu kuwani nafasi ya mwenyekiti wa
wilaya hiyo ni Mussa Ntimizi ,Hamisi Bundala na Abdallla Kazwika ambaye natetea
nafasi yake ya kiti.
Katika
wilaya Igunga katibu wa wilaya hiyo Mary Maziku aliwataja waliochukua fomu hizo
kwa nasafi ya wenyekiti wa wilaya hiyo ni Costa Olomi na Felix Mkunde.
Nzega
aliyekuchukua fomui hizo ni Patric Bulubuza pekee hadi leo hiyo sikonge aliyechukua
nafasi hiyo fomu za kuwania nafasi ya wenyekiti Abed Malifedha ambapo kwa Tabora mjini aliyechukua fomu hiyo
ni Simon Madolu .
Mwisho
No comments:
Post a Comment