NA LUCAS RAPHAELTABORA
MAKALA YA MICHEZO.
“ili kiwango cha michezo mkoani Tabora
kiweze kukua wanatakiwa wapatikane viongozi watakaojitoa kwa hali na mali kwa
ajili ya kuendeleza soka la mkoa wa huo.
Kusimamia michezo kwa vitendo ,kukuza vipaji
na kuwa na mbinu mbadala kwa ajili ya kukuza viwango vya michezo mbalimbali
ya mpira wa miguu wa wananwake ,watoto na watu wazima wenye umri wa miaka 20
hadi 25.
Bila ya kuchaguliwa kwa na viongozi bora
wenye nia ya dhati ya kuendeleza soka la mkoa huu, tena wenye
uwezo wa kujitolea na kuendeleza michezo mkoani hapa,katu kiwango cha mpira
hakitafanikiwa kukua kama ilivyokuwa miaka
20 iliyopita”
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa mkutano
mkuu wa TFF kutoka mkoani Tabora, Yussuf Kitumbo katika mahojiano maalum na
gazeti hili,amesema kwamba wakati umefika mkoa wa Tabora kuchangua viongozi
watakaokuwa tayari kujitolea kwa ajili ya soka la mkoa huu.
Amesema kwamba katika kipindi cha kupata
viongozi wa wilaya hakikishe wanapata viongozi wanaopenda michezo ili kujenga
timu bora ya uongozi katika kukuza kiwango cha soka mkoani Tabora kwa kipindi
cha miaka minne ijayo.
Amesema kuwa umefika wakati sasa wa
kuhakikisha soka la mkoa linakua ili kuweza kurejea rekodi ya miaka iliyopita
ambayo soka linakuwa bora na kuweza kuwatoa wachezaji bora kwenye timu ya
mkoa na timu ya Taifa .
Kitumbo amesema kwamba kwa kipindi hicho
cha kuelekea kwa uchaguzi huo wa TAREFA basi hakuna budi kuhakikisha viongozi
wanachaguliwa kuongoza vyama vya michezo wilayani wawe wakereketwa wa michezo
kwa maana ya kujitolea kwa hali na mali katika maswala ya michezo .
Amesema kwamba bila kuwa na uongozi mzuri
katika vyama vya michezo ndio chanzo kikubwa cha kushuka kwa kiwango cha soko
mkoani hapa .
Amesema kuwa wakipatikana viongozi wazuri
katika vyama hivyo na kufanya kazi kama timu ya ushindi, ushindi utapatina
kwa ushirikiano bila kuwepo kwa makundi ,soka la Tabora litakuwa na mafanikio
yatakayonekana.
Amesema kwamba viongozi hao wakipatika na
kuongoza vizuri vyama vya soka na chama cha soka mkoa wanaweza kufanya vizuri
katika kukuza soka la mkoa wa Tabora.
Mjumbe huyo wa mkutano mkuu wa Tff
amendelea kusema kwamba dawa ya kukuza soka la mkoa ni kupata viongozi wenye
nia ya dhati ya kukuza kiwango cha mpira wa miguu na kukuza vipaji kwa vijana
chini nya miaka 13,15 na 17.
“Viongozi watakao changuliwa warejeshe
imani kwa wadau wasoka ili waweze kujitokeza kuzichangia timu za mkoa
zinazoshiriki katika michezo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa huo”amesma
kitumbo.
Amesema kwamba wadau wa michezo hawaoni
nini wachangia kwani uongozi wa chama cha
soka mkoa wa Tabora ,TAREFA umeshindwa kufanya kazi kama
timu ili kuweza kuwavuta wadau wa soka ambao wapo tayari kuchangia maendeleo ya
soka .
Amesema kwamba lazima viongozi wanaopata
nafasi ya kukiendesha chama cha soka mkoa wa Tabora wahakikishe
wanarudiasha imani kwa wadau kwenye mchezo wa mpira wa miguu”
Amesema kwamba hilo likifanyika tutakuwa tumeishirikisha
jamii nzima
kwenye soka ambapo mwisho wa siku watakuwa na uwezo wa kuchangia soka mkoani
hapa.
Amesema hali hiyo inatokana na viongozi
wa mkoa wa cha soka umedhamirie kukuza kiwango cha mpira mkaoni Tabora kuwa
timu zake zote zinafanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Kitumbo amesema kwamba chama chochote cha
soka kama akina mipango madhubuti ya kuendeleza soka ni lazimakitakuwa
akina dira wale mwelekeo wa badaye , chama kiwe na fedha kwa ajili ya
kuzisaidia timu ambazo zinashiriki katika mashindano mbalimbali.
Akizungumzia swala la vyama kukosa
mipango na ukosefu wa fedha na kushindwa kuzisaidia timu zinashirikia
katika michezo mbalimbali amesema tatizo hilo linasababishwa na viongozi
kutojitoa katika kukuza soka la sehemu husika na kushindwa kupandisha hata
daraja, hawana mipango endelevu ya michezo.
Amesema kuwa iwapo cha cha soka cha
sehemu husika kikiwa na mikakati madhubuti ya kupata fedha na kiaminika
akiwezi kushindwa kukosa fedha kwa ajili ya kuisaidia timu ambayo inashiriki
katika mashindano ndani na nje ya mkoa wa Tabora.
Amesema kwamba mkoa wowote upate timu
zinashirikia katika ligi daraja la kwanza kama ilivyotokea kwa mkoa wa Tabora
huko morogoro,iwapo chama kingikuwa na fedha za kutosha timu hizo zingeweza
kufanya vizuri.
Amesema ni lazima tuvisaidie vilabu
kimkakati kwa maana ya kujipanga lengo likiwa ni kupata timu itakayoshiriki
ligi ya voda com na wilaya nazo ziwe na mikakati ya kuhakikisha kupandisha
timu daraja Fulani hayo yote ni mikakati ya chama cha soka cha mkoa .
“Lakini chama cha soka wilaya na
mkoa hawana mipango endelevu yenye
lengo la kukuza kiwango cha soka ”amesema kitumbo .
Hata hivyo amesema kwamba mipango mingine
ya chama cha soka kwa viongozi wanaotaka nafasi ya kuongoza vyama vya soka
kuhakikisha wanasimamia soka la watoto wadogo ili kesho na keshokutwa TAREFA
wawe na wachezaji katika vilabu vinavyoshiriki ligi
kuu ikiwemo AZAM,YANGA na SIMBA.
AIDHA amesema kuwa Tabora kuwepo na kituo
cha michezo kwa ajili ya kukuza vipaji vya watoto hasa wanaoshirikia Copa coca cola.kichosimamiwa na chama cha soka
mkoa wa Tabora .
Haya yote yanaweza kufanikiwa kukuza
kiwango cha soka mkoani hapa iwapo wanamichezo wataondokana na
malumbano mbayo yanachangia kwa kiwango kikubwa kudidimiza soka .
Licha ya hivyo viongozi kushindwa
kuonesha mshikamano wakuendeleza soka la mkoa wa Tabora na kusababaisha hata
wadau wa michezo kushindwa kushirikiana na chama hicho kwa kukosa imani na
viongozi waliopa madarakani.
Wadau mbali mbali wa soka mkoani hapa
wamempongeza mjumbe huyo kwa kujitole kuendeleza soka la mkoa huu licha ya
kuwepo kwa malumbanao kwa baadhi ya viongozi .
Wadau hao wamesema mdau huo wa soka
amekuwa akujitolea kuzichangia timu za Polisi na Rhino Rangers za
mjini hapa ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza pamoja na timu ya
Majimaji ambayo ni bingwa wa mkoa kwa msimu uliopita.
Mwisho
No comments:
Post a Comment