NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
HABARI ZA MKOA WA TABORA
HISA IGUNGA.
MWENYEKITI
wa bodi ya mamlaka ya maji wilaya ya Igunga Costa Olomi ,mkuu wa wilaya ya
Igunga Elibaiki Kingu na Sharifa Said,
wameteuliwa kuwa walezi wa wa
jumuiya ya hisa na maendeleo
wilaya ya Igunga, ili wavilee vikundi vya hisa kwa lengo la kufikisha maendeleo kwa wananchi
wa wilaya hiyo.
Akiwaapisha walezi hao,
mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu akifunga mkutano mkuu wa
jamuiya hiyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya
kuhakikisha Igunga inasonga mbele.
Alisema kwamba maendeleo ya wanaigunga yatajengwa na wana
Igunga mweyewe kwa maaana hiyo watu wa
wilaya ya hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa biidi ili kujiletea maendelo yao wenyewe katika nyanja
mbalimbal za kiuchumi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba anataka wilaya ya
Igunga iwe mfano wa wilaya nyingine
mkoani Tabora, katika kuimarisha kilimo
cha chakula na biashara na kuwezesha wakulima kulima na kupata ziada licha ya
wilaya hiyo kuwa na uchache wa mvua .
Hata hivyo baada ya Jumuiya hiyo kupata walezi Costa Olomi alikubalki kuwatumikia wananchi
hao, ili kufanikisha maendeleo ya
wananchi hao kwa nguvu zote .
Alisema kwamba amekuwa mlezi wa kikundi hicho toka mwaka 2007 kwa kuvikusanya vikundi
mbalimbali kutoka kikundi kimoja hadi kufikia vikundi 260 vyenye watu 7000 na
bado kwa imani hiyo jumuiya hiyo kuona mchango wake ameamua mteue rasmi kuwa
mlezi wa kikundi hicho.
Sharifa Said alisema kwamba amefurahishwa kukufanya kazi kwa karibu na mkuu wa wilaya
hiyo kwani anonekana ni mchapa kazi na mtu mwenye
mkakati wa kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Igunga .
MWISHO.
MATREKTA.
Halmashauri
ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora inatoa matrekta 12 yenye thamani ya shilingi
milioni 450 kwa kata 12 za wilaya ya hiyo kwa ajili ya kusaidia kukua kwa
uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara na hatimaye kukuza kipato cha
wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Elibariki Kingu,
aliwataka wakulima kuhakikisha kwamba wanayatumia vizuri matrekta hayo kwa
lengo la kuinua uzalishaji na hivyo kuwa na uhakika wa kipato.
Aliwataka wakulima kuongeza ukubwa wa mashamba yao na
kuhakikisha kuwa wanayatumia matrekta hayo kwa lengo la kupambana na umasikini
kwa kufanyakazi kama watumwa tena bila
ya kuchoka kwa ajili ya manufaa ya familia zao.
Alisema wakumbuke kuwa matrekta hayo yanayotarajiwa kununuliwa
na Halmashauri hiyo hayatolewi kama zawadi bali ni mkopo na hivyo watatakiwa
kuurejesha mara baada ya kuanza kuuza mazao yao kulingana na mkataba.
Alisema ofisi ya mkuu wa wilaya itaingia nao mkataba kwa lengo
la kuhakikisha kuwa vikundi hivyo vya ujasiliamali vinaimarika na vinapata
uwezo wa kurejesha mikopo hiyo kulingana na mkataba baina yake na Halmashauri
ya wilaya hiyo.
Kwa upande wa
wafanyabiashara wadogo wadogo
waliopo kwenye mji wa Igunga, Mkuu wa wilaya aliwataka wajiunge pamoja
na kuchagua uongozi wao ili waonane na viongozi wao na kisha kuandaa utaratibu
wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo.
Alisema lengo la serikali na halmashauri ya wilaya ya Igunga
ni kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara
bila ya kuwasahau wafugaji kuboresha hali zao za maisha kwa kujenga
nyumba nzuri za kuishi na kusomesha
watoto.
Mwisho.
Camartec.
Wakulima mkoani Tabora wamekishukuru kituo cha zana za kilimo
nchini na ufundi vijijini (CAMARTEC) kutokana na kuonyesha vifaa vya kisasa
vyenye kukidhi mahitaji halisi ya matumizi ya zana hizo katika maeneo ya
vijijini.
Wakulima
hao walitoa shukrani hizo walipotembelea banda la maonyesho
la CAMARTEC katika viwanja vya
Nane nane vilivyopo kwenye eneo la Ipuli mjini Tabora, ambapo walijionea zana
mbali mbali za kilimo zinazotumia teknolojia ya kisasa.
Mkulima wa Tumbaku na
Mahindi mkoani Tabora, Shaaban Ntahondi,
alifurahishwa sana na mashine ya kisasa ya kupuchukua mahindi ambayo imetengenezwa na CAMARTEC ambapo kwa
mujibu wa wataalam wa kituo hicho inauwezo wa kupuchukua gunia tano za mahindi
kwa saa.
Alisema mashine hiyo itawasaidia wakulima wengi kuepukana na matumizi ya kupiga mahindi,
ambapo licha ya kutumia idadi kubwa ya watu lakini bado imekuwa haina ufanisi
wa kutosha na gharama za kuwalisha watumishi bado ni kubwa.
Alisema pamoja na teknolojia hiyo pia mtambo wa kuchemsha maji
kwa kutumia umeme wa jua pia itawasaidia wakulima kuachana na matumizi ya kuni
ambazo alisema zimekuwa zikileta madhara makubwa kwa binadamu na viumbe hai
kutokana na kumaliza miti.
Mkulima mwingine Hassan
Wakasuvi, alifurahishwa na teknolojia ya matrekta yaliyotengenezwa na CAMARTEC
ambayo licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kulima pia yamekuwa yakitumia majembe
tofauti tofauti kwa ajili ya kulima, kupanda, kuvuna na kuchambua mazao kwa
uhakika.
Alisema kwa ubunifu kama huu tunaweza kumkomboa mkulima wa Tanzania,
akaondokana na kilimo cha jembe la mkono ambacho hakina tija na kuweza
kujikomboa na kuzalisha mazao mengi zaidi hivyo kuweza kuondokana na njaa.
Aliwataka wakulima wawe wanatembelea manesha ya nane nane kila
mwaka kwani yanafaida kubwa kwao kwa
kuona na kupata nafasi ya kuitumia teknolojia mpya zinazozalishwa na wataalam
ambazo alisema zitasaidia kuwaondoa katika hali duni.
Katika maonesho hayo CAMARTEC ilioonyesha bidhaa mbali mbali
za zana za kilimo ambazo zimebuniwa na kutengenezwa na wataalam wake, kama mashine
ya kukamua mafuta, majiko ya biogas, Matrekta, majembe ya kilimo cha wanyama
kazi, majiko banifu na sanifu ya mkaa, Mashine ya kumenya karanga, mashine ya
mashine ya kukamua mbegu za mafuta na kadhalika.
Afisa Masoko wa
CAMARTEC Lambart Rwebangira na Meneja wa CAMARTEC tawi la Nzega, mkoani Tabora,
Mkoko Yassin walisema kuwa taasisi hiyo
imekuwa ikibuni zana mbali mbali kwa kutumia teknolojia rahisi ambayo
itawasaidia wakulima kuboresha maisha yao na kulisaidia Taifa kuondokana na tatizo la njaa na ukosefu
wa fedha za kigeni kwa kuuza mazao yao nje
ya nchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment