Na Lucas Raphael,Tabora
Mwenyekiti.
Baraza la madiwani la Madiwani la
Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, limemchagua diwani wa kata ya
Ilolangulu katika wilaya hiyo, Said Shaaban Ntahondi, kuwa kuwa mwenyekiti
wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mwaka 2015 utakapofanyika
uchaguzi mkuu nchini.
Katika kikao chake kilichofanyika makao
makuu ya wilaya hiyo mji mdogo wa Isikizya na kuhudhuriwa na madiwani wote 29
wa halmashauri hiyo, madiwani hao walimchagua diwani Said Shaaban
Ntahondi, kuiongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu
.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Doroth Rwiza, alisema Ntahondi
amepata kura 29 kati ya kura 29 zilizopigwa na hivyo kuwa mwenyekiti wa
halmashauri hiyo.
Diwani Ntahondi, amechaguliwa kushika
nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mashaka
Kalyuwa, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na majambazi nyumbani kwake Ipuli mjini
Tabora, Mwanzoni mwa Mwaka huu.
Aidha Kikao hicho kwa kauli moja
kilimchagua diwani wa Igalula, Seleman Kapalu kuwa makamo mwenyekiti wa
halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kapalu alipata kura 29 kati ya
kura 29 zilizopigwa na madiwani wa halmashauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa,
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Ntahondi, alisema kuwa atajitahidi
kuiongoza halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na kwamba
anachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa madiwani na watumishi.
Alisema kwamba bila ushirikiano kati ya
wataalam na madiwani kazi kwake itakuiwa ni ngumu kwanio umajo na mashikamano
utakuwa ni ndogo ,hivyo rai yake kubwa ni kupata ushirikiano kutoka sehemu zote
mbili na tatu kwa viongozi kuwatumikia wananchi kwa nguvu na kasi.
Ntahodi kabla ya kupata nafasi hiyo alikuwa
ni makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo na mara baada ya kufariki mwenyekiti
wake aliongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miezi 4.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment