mfugaji tabora apiga mkulima,ajeruhi pia adai polisi kaiweka mfukoni
MKAZI kijiji cha Lunguya,kata ya Upuge,wilayani Uyui,mkoani Tabora,Moshi
Shaban Chimagula,(54),amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa na mfugaji
aliyetajwa kwa jina la Jilala Peter,baada kushambuliwa na fimbo sehemu
za mwili wake akizuiwa kulisha mifugo yake katika shamba hilo.
Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio hilo,Chimagula alisema hivi
sasa ameruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni,mbavu na
kifuani na alipatiwa PF 3 na kwenda kutibiwa hospitali ya mkoa wa
Tabora Kitete.
Chimagula alifafanua kuwa tukio hilo lilimtokea majira ya saa 11:00
jioni,mnamo mwezi agosti 3,mwaka huu,akiwa nyumbani kwake alipata
taarifa kuwa bustanini kwake kuna mfugaji aliyetajwa kwa jina la Jilala
analisha mifugo yake na ndipo alipoamua kwenda kumuondoa.
Alisema alipofika na kujaribu kumuondoa alianza kushambuliwa kwa
fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake,ikiwemo tumboni,mbavuni na
kichwani hali ambayo imepelekea kuendelea kupata matibabu hadi sasa huku
mbavu na kifua bado vikiwa na matatizo.
Mkazi huyo alifafanua zaidi kuwa alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa
kijiji Lunguya aliyemtaja kwa jina la Peter Mahanga,ambaye alimpatia
barua ya kwenda kutibiwa,barua ambayo iliandikwa mnamo mwezi agosti
4,mwaka huu.
Alisema baada ya kupewa barua hiyo alikwenda kituo cha afya cha kata
ya Upuge,lakini alijibiwa aende hospitali ya mkoa wa
Tabora,Kitete,ndipo alipofunga safari na kuanza matibabu yake hadi sasa
na baada ya picha ya X-Ray aligundulika ana hitilafu kwenye mbavu zake
na kifua.
Aidha kabla ya kwenda hospitali alipitia polisi na kufungua kesi ya
shambulio iliypewa namba,UY/RB/594/2012,na alipewa PF 3 iliyojazwa na
askari WP 9019 PC Johari,lakini hadi sasa mfugaji huyo hajakamatwa na
yeye bado ana maumivu makali.
"Kinachonishangaza ni polisi kushindwa kumkamata mtuhumiwa huku mimi
nikiwa natishiwa maisha na mfugaji huyo kuwa nitauawa,na mwenyekiti wa
kijiji hicho anayo taarifa lakini wamekaa kimya hadi sasa.
Aliema
hadi sasa maisha yake yapo hatarini kwani anatishiwa kuuawa na mfugaji
huyo na zaidi shamba lake ambalo analima nyanya,matango,matikiti
maji,kabeji,mchicha na spinachi,sehemu kadhaa imechomwa moto.
"Nimefanya juhudi kuuelezea uongozi wa kijiji,wakiwemo polisi lakini
hadi sasa ni kimya na mimi naendelea na kutishiwa maisha,kazi sasa
katika shmaba langu nimesimama kutokana na maumivu ambayo yanaendelea."
alisema.
Alisema kila anapofuatilia kesi yake anapigwa danadana na zaidi hata
mwenyekiti wa kijiji cha Lunguya,Paulo Mahanga,alimtamkia OCD wa wilaya
ya Uyui,kuwa anashindwa kumkamata mtuhumiwa kwani ni tishio sana pale
kijijini.
Chimaguli ameiomba serikali ya mkoa wa Tabora kumsaidia kwani
vitisho dhidi yake vinaendelea,na amekuwa akiishi kwa hofu kubwa kila
anapotaka kuchukua hatua zaidi na hana msaada wowote kwani hata uongozi
wa kijiji unamgwaya mfugaji huyo.
Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha Lunguya,Paulo
Mahanga ambaye alikiri kuwepo kwa tukio hilo na yeye alishatoa barua kwa
mhanga kwenda kutibiwa na zaidi yeye yupo tayari kutoa ushahidi
mahakamani endapo kesi hiyo itahitajika kufanya hivyo.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alikana kuwa mfugaji huyo anatikisa
kijiji hicho na anaogopwa hata kufunguliwa kesi ya jinai,na kusisitiza
kuwa polisi wanayo taarifa juu ya tukio hilo la mwananchi wake kuumizwa.
Aidha
alikiri ni kweli bustani na shamba la mwananchi Chimaguli lililishiwa
mifugo na bwana Jilala ikiwemo sehemu kadhaa kuchomwa moto,ambapo
alitamka kuwa yeye ni mwenyekiti tu hawezi kumkamata mfugaji huyo.
Naye mfugaji Jilala Peter alipotafutwa kwa njia ya simu kujibu
tuhuma hizo alikata simu na kuizima kabisa akiwa malishoni na jitihada
zilifanyika kumpata haikuweza kujulikana yupo sehemu gani.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Tabora Anton Rutta alipotafutwa na gazeti hili
alisema suala hilo halijamfikia mezani kwake na kuahidi kulifuatilia ili
kama kuna ukweli hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake
kukomesha tabia hiyo.
Mwisho-
No comments:
Post a Comment