Na. Mwandishi
wetu
SHIRIKA la Mtandao
wa Maendelea wilaya ya Uyui mkoani Tabora (UCODEN) linatarajia kutumia shilingi
milioni 30 kwa ajili ya kufanya midahalo mbalimbali kwa wananchi ili kuwajengea
ujasili wa kutoa maoni yao bila woga, kuhusu madiliko ya katiba mpya.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti
wa Shirika hilo, Ally Magoha wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa, kuhusiana na kazi hiyo watakavyoifanya katika kipindi cha mwaka mmoja.
Magoha alisema kwamba lengo
kuu la midahalo hiyo ni kuwajengea ujasili na uwezo wananchi ili wakati ukifika
wakutoa maoni kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya watoe maoni yao
bila ya woga wowote jinsi ambavyo wanataka katiba iwe na muundo upi.
Alieleza kwamba iwapo wananchi
watajengewa uwezo huo bila shaka katiba itayoundwa itakuwa na tija zaidi kwa
wananchi kuliko ilivyo sasa katiba hiyo haiwapi uhuru wa kufanya mambo yao ya
msingi.
“Midahalo hiyo itawajengea
ujasili wananchi juu ya kuwahoji wajumbe wa tume ya kukusanya maoni
kuhusu katiba mpya pia nao kutoa maoni wanahitaji katiba hiyo iwe na muundo wa
namna gani”alisema Magoha.
Kwa upande wake Mratibu wa
Shirika hilo ,Christopher Nyamwanji alisema kuwa lengo lingine la kufanya
midahalo hiyo pia ni kukuza mahusiano kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.
Nyamwanji pia alisema
midahalo hiyo pia italenga kutoa elimu kwa wananchi hao, kuhusu tabia
nchi na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanapelekea kwa sasa katika baadhi ya
mikoa hapa nchini mvua kutonyesha kwa wakati.
Alisema kama uhusiano
utakuwawepo baina ya wananchi na viongozi kazi za miradi mablimbali ya
maendeleo zitasonga mbele na kwamba midahalo inatarajiwa kufanyika katika
vijiji vya Igalula na Goweko wilayani Uyui.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment