Monday, May 12, 2014

"BASHE ANG'ARA ZIARA YA KINANA WILAYANI NZEGA,WATU WAMSHANGILIA KILA ANAPOTAJWA"

20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Abdulrahman Kinana akimpongeza mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Bw. Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi kwa viongozi wa kata  pikipiki kwa ajili ya watendaji wa chama cha Mapinduzi.
Katibu mkuu wa CCM Bw.Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kada wa CCM Bw.Hussein Bashe wakati akitamka na kutoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata mojawapo huko wilayani Nzega ambapo Bw.Kinana alifanya ziara ya siku mbili kwa ajili ya kuangalia uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa wananchi.
KIAPO
Kada wa Chama cha Mapinduzi Bw.Hussein Bashe akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kampala iliyopo wilayani Nzega,ambapo wanafunzi hao walionesha kumshangilia sana kwa kile kinachodaiwa kuwa Bashe amekuwa karibu sana na Shule hiyo katika kukabiliana na Changamoto za elimu kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
10 Mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala akimpongeza Mjumbe wa mkutano mkuuu wa CCM Bw. Hussein Bashe mara baada ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Nkiniziwa, katikati ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.

No comments:

Post a Comment