Thursday, May 29, 2014

KAMPUNI YA UNUNUZI YA ALLIENCES ONE YATOA MSAADA WA MAWADAWATI



NA LUCAS RAPHAEL
AFISA MAHUSIANO WA KAMPUNI YA ALLIENCES ONE HAMIS LIANA AKIONGEA NA WALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA MADAHA WILAYA YA UYUI WAKATI AKIKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 75

AFISA MAHUSIANO HAMIS LIANA AKIMKABIDHI MWENYEKII WA HALMASHAURI YA WILAYA YA UYUI SAID NTAHONDI MADAWATI 75 YALIYOTOLEWA NA KAMAPUNI YA UNNUZI WA TUMBAKU MKOANI HAPA YA ALLIENCES ONE KWENYE  SHULE YA MSINGI YA MADAHA KIJIJI CHA MPENGE WILAYA YA UYUI


BAADHI YA WANANFUNZI WA SHULE YA MSINGI MADAHA KATIKA KIJIJI CHA MPENGE KATA YA ILOLANGULU WAKISIKILIZA WAGENI WALIOFIKA KUTOA MSAADA WA MADAWATI KWA AJILI YA KUPUNGUZA UHABA WA MADAWATI KATIKA SHULE HIYO

Kampuni ya ununuzi wa tumbaku ya Allience One imetoa msaada wa madawati 75 yenye thamani ya shilingi milioni 4,875,000/= katika shule ya msingi Madaha iliyopo katika kijiji cha Mpenge kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora.

Akikabidhi msaada huo Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Hamis Liana amesema msaada huo wa madawati utasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Alisema msaada huo wa madawati uwe chachu kwa walimu kuongeza juhudi za kufundisha na wazazi kujikita zaidi katika shughuli za kilimo kwa kuwa wamepunguziwa mzigo wa kuchangia ununuzi wa madawati katika shule hiyo.

Liana alibainisha kuwa kampuni ya Allience one imejiwekea mkakati wa kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu kwa kutoa madawati na vitabu.

Afisa huyo mahusiano alisema kampuni yake imekuwa ikichangia katika miradi hiyo katika maeneo ambayo wananunua tumbaku kupitia vyama vya msingi vya ushirika ambavyo vinaiuzia tumbaku kampuni hiyo.

“Wakulima kupitia vyama vya msingi wamekuwa wakionesha jitihada za kuwauzia tumbaku, hivyo nasi tunalazimika kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao”. Alisema Liana.

Akipokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Catherine Mmbando alisema anashukuru kwa kupata msaada huo wa madawati kwani umeondoa tatizo la upungufu wa madawati katika shule hiyo.

Alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 71 lakini kampuni hiyo imefanikiwa kuwapatia madawati 75 ikiwa ni zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya shule.

Mwalimu huyo alisema shule yake yenye jumla ya wanafunzi 391 na walimu 13 kwa pamoja watahakikisha wanatumia madawati hayo kwa uangalifu ili yaendelee kuleta tija kitaaluma shuleni hapo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment