Sunday, June 15, 2014

TIMU YA WAPELELEZI MAKAO MAKUU YA POLISI WATINGA TABORA KUWASHUGHULIKIA VIONGOZI WABADHIRIFU KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA TUMBAKU


Issaya Mngulu – CP
Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI)



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 11/06/2014

IGP ATEUWA TIMU YA WAPELELEZI KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WIZI KATIKA VYAMA VYA MSINGI MKOANI TABORA.

Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi Tanzania kutokana na maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya muungano na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliyoyatoa tarehe 07/06/2014 ya kuagiza timu ya upelelezi kutoka makao makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya kuchunguza wizi unaofanywa na vyama vya msingi kwa wakulima wa Tumbaku, timu hiyo imeshawasili mkoani Tabora.

Timu hii inaongozwa na Kamishna wa Polisi – Issaya Mngulu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania.  

 Kama alivyoagiza Rais, timu hii maalum imekuja mahususi kwa ajili ya kuchunguza wizi wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya msingi mkoani Tabora. Hivyo timu hii inaanza kazi mara moja kwa kuchunguza chama kimoja hadi kingine ili kuweza kubaini wizi na hujuma zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika ambazo ni kero kwa wakulima wa tumbaku katika mkoa wa Tabora.

Natoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu hii mara wanapohitajika ili kuweza kukamilisha kazi yake.
Imetolewa na:-
Issaya Mngulu – CP
Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI)

No comments:

Post a Comment