Sunday, June 15, 2014

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TABORA




 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF nchini Balozi Ali Mchumo akizungumza na Wadau wa mfuko huo ambapo alisema NHIF imekusudia kuboresha mfuko huo ili kuondoa kero kwa wanachama  hususani upatikanaji wa dawa.
Mgeni rasmi katika Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Tabora Bw.Elibariki Kingu ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tabora,Mkutano uliofanyika katikaukumbi wa Isike Mwanakiyungi ambapo wadau walikuwa wakijadili Changamoto mbalimbali ikiwa na lengo la kuboresha mfuko huo kwa wanachama wake.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Hamisi Mdee akielezea malengo ya mkutano huo wa wadau ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza wadau kujitokeza kufungua maduka ya dawa muhimu vijijini ambayo yatasajiliwa  NHIF na yatakuwa yakitoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua akizungumza katika mkutano huo
Meneja wa NHIF kanda magharibi Bw.Emmanuel Adina akitoa maelezo mafupi kuhusu mfuko huo kwa kanda ya magharibi.



Baadhi ya viongozi na wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wa mkutano wa Wadau ambao unalengo la kujadili Changamoto mbalimbali zinazoukabili Mfuko huo. 






SERIKALI mkoani Tabora imewaagiza viongozi na watendaji wote huduma za mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kuwa ajnda za vikao vyote vya maamuzi.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa kwenye mkutano wa siku ya wadau wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) uliofanyika ukumbi wa mtemi Mwanakiyungi.

Akisoma taarifa kwa niaba ya mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya ya Igunga Elibariki Kingu alisema mkoa wa Tabora unaonyesha takwimu hadi kufikia mwezi machi 30 mwaka huu ni kaya 39,969 sawa na asilimia 11 zimejiunga na CHF kati ya kaya 379,268 zilizopo mkoani Tabora.

Kingu aliongeza takwimu hizo zinaonyesha kuwa viongozi mkoani hapa bado hawajatimiza wajibu kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko.

Aidha alisema kwa upande mwingine watoa huduma wamekuwa chanzo cha wananchi kukata tama kujiunga na CHF huku wananchi wengine wakisita kujiunga na mfuko kutokana nap engine kuwepo na huduma hafifu.

‘Ipo haja ya kuangalia kwa umakini ni kwani kunakuwepo na kuzorota kwa utaratibu hu ambao baadhi ya halmashauri hapa nchini umeimarika.’ alisema.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwaasa watoa huduma kufanya kazi zao kwa weledi na bila ubaguzi wowote kwa wananchi kwani mojawapo ya malalamiko ya wananchi ni kukithiri kwa hali ya ubaguzi.

Aidha aliwaomba wanachama wa NHIF na CHF kutumia kadi za matibabu kwa kuzingatia taratibu zilizopo na kuacha tabia ya kuhamishana kadi au kufanya biashara ya kadi hizo.

Mwassa aliwaomba watumia wa NHIF kutimiza wajibu wao bila woga wakati wowote pale wanapohitajika na kuwataka kushirikiana na serikali kutatua changamoto za mfuko kwa pamoja.
Mwisho-

No comments:

Post a Comment