Tuesday, June 17, 2014

MGOGORO WA WAISLAMU TABORA:-ALIYEKUWA SHEIKH MKUU AFIKISHWA MAHAKAMANI,AACHIWA KWA DHAMANA

NA LUCAS RAPHAEL,TABORA.

 
Shehkh wa mkoa wa Tabora Salum Shaban Salum  na waumini wenzake wa dini ya kiislam watano wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wakikabiliwa na shitaka la kutishia kufanya fujo.
 
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mkoa wa Tabora Issa Magoli ilidaiwa na wakili wa serikali Juliana Changalawe kuwa watuhumiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo tarehe 14/06/2014 katika msikiti mkuu wa mkoa uliopo eneo la Gongoni mjini hapa.
 
Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo majira ya mchana watuhumiwa Shaban Salum, Mgude Ahmed, Said Maganga, Kassim Shomary, Abubbakar Ludenga na Kassim Rajab walimtoa sehemu ya ibada  Shehkh Ibrahim Mavumbi.
 
Watuhumiwa ambao wanawakilishwa na wakili msomi Mussa Kwikima wa miji hapa mara baada ya kusomewa shitaka hilo waote walikana na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30/06  kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwani upelelezi umeisha kamilika na wote walipata dhamana.
 
Kukamatwa hadi kufikishwa mahakamani kwa shehkh huyo na wenzake kunafuatia mgogolo ambao umekuwa  ukiendelea na kupelekea Mufti wa Tanzaniia  Shaban Simba kutangaza kumuengua shehkh wa mkoa wa Tabora
Shaban Salum kitendo ambacho kinapingwa na baadhi ya waislamu.
 
Katika mgogolo huo baadhi ya waislamu wanapinga uhamzi huo ambapo Mufti alimtangaza shehkh Mavumbi Ally kuwa kaimu shehk wa mkoa wakati kwenye uchaguzi alishindwa .
 
Hata hivyo habari kutoka ndani ya waumini wa dini ya kiislam mkoani hapa wanadai kuwa mgogolo huo unachochewa na viongozi wa serikali ambao wanalazimisha shehk mavumbi ndiye awe kiongozi wa mkoa wa dini hiyo.
 

Aliyekuwa Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora Sheikh Shaaban Salumu(aliyevaa shati jeusi) wakati alipokuwa barabarani akisindikizwa na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kuachiwa kwa dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Tabora akituhumiwa kwa kosa la kutaka kuleta fujo msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mjini Tabora  akiwa na waumini wengine watano.
Sheikh Shaaban Salum akiwa na baadhi ya waumini waliounganishwa naye katika kesi moja mahakama ya hakimu mkazi Tabora mjini.

No comments:

Post a Comment