Thursday, May 8, 2014

RAGE AZOMEWA MBELE YA JANUARI MAKAMBA,KISA MJADALA WA KATIBA KUINGIZA LIGI YAKE BINAFSI

Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mheshimiwa Ismail Aden Rage akizungumza katika kongamano la Katiba lililohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Tabora.
Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Bw.Januari Makamba akisikiliza namna ambavyo wanafunzi wa vyuo vikuu walivyokuwa wakimzomea mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mheshimiwa Ismail Rage.
Wanafunzi vyuo vikuu Tabora mjini
Na Lucas Raphael Tabora



Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Aden Rage amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wanafunzi wa Umoja wa Vyuo Vikuu mkoani Tabora.

Rage alipatwa na mkasa huo kwenye Kongamano la vijana kuhusu rasimu ya katiba lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu August(SAUT)tawi la Tabora ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba.

Katika Kongamano hilo baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vya SAUT,THEOFILO KISANJI,CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA,MUSOMA UTALII NA TABORA NETWORK walianza kumzomea mbunge huyo baada ya kuwaeleza anataka kuanzisha Ligi ya mpira wa miguu RAGE CUP.

"Nataka nijitambulishe kwenu nafasi yangu nyingine mimi ni Mwenyekiti wa Simba pia nataka nianzishe mashindano ya Rage cup katika vyuo kumi na moja ili wapate timu ya mpira iliyo bora hapa kwetu,au mnasemaje vijana?...alisema Rage

Baada ya kusema hivyo tu ndipo aliamsha kelele kubwa kwa wanafunzi hao huku wakimtaka akae kimya na wengine wakimtaka aondoke ukumbini kwakuwa kikao hicho inasemekana Rage alidandia.

"Nenda kawaongoze Simba sisi hatukutaki,kwanza hapa tunaongelea masuala ya msingi ya Katiba sasa wewe unatuletea mambo ya mpira nenda bwana,kwanza hujui hata thamani ya maisha ya mtanzania,na tutaona wakati wa uchaguzi mkuu labda CCM wampange mtu mwingine lakini wewe tunauhakika watapoteza jimbo"walisikika wakisema hayo.

Hatua hiyo pia ilienda samabamba na kumweleza  mbunge huyo kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi bungeni ikiwa ni pamoja na kutokuwa na muda wa kusikiliza kero za wananchi akiwa jimboni kwake.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya alilazimika kuingilia kati sakata hilo lililokuwa likifanyika mbele ya Naibu waziri January Makamba ambapo aliwasihi wanafunzi hao kuto zomea juhudi ambazo ziligonga mwamba  hadi wanafunzi hao walipoacha wenyewe kwa kutulizwa na viongozi wao.

"Hivi mnavyofanya zomea zomea mimi nasema kama kiongozi wa Serikali si sahihi hata kidogo,mnatakiwa muwe wavumilivu na kusikiliza na kujenga hoja na siyo kuzomea" alisema kumchaya 

"Hata tukizomea wewe inakuhusu nini mbona Wabunge wanazome na wanalipwa laki tatu kwa siku bungeni,sisi tumeamua kuzomea bila malipo tatizo liko wapi mtu kujitolea bila malipo kukomesha uongo wa viongozi  wasio waadilifu"walisikika tena wakimjibu mkuu wa wilaya katika ukumbi huo.

     

No comments:

Post a Comment