Bw.Mwakasaka akikabidhiwa Usinga wa Kiswezi(kifaa cha matambiko)na mkuki ikiwa ni ishara ya kutawazwa kuwa kiongozi mlezi wa Waswezi Tabora. |
Friday, January 31, 2014
"MWAKASAKA AMRITHI MWALIMU NYERERE"
RAIS KIKWETE AMPIGA KIJEMBE RAGE
RAIS Jakaya Kikwete amemshangaa
Mwenyekiti wa Simba SC ya jijini Dar es Salaam, Ismail Aden Rage kwa
kuitisha mkutano wenye ajenda moja kwa ajili ya wanachama wa klabu hiyo.
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Simba Rage, alitangaza kuwepo kwa mkutano
wa klabu hiyo Machi 23 na kueleza wazi kuwa kutakuwa na ajenda moja ya
kujadili mapungufu ya Katiba.
Akizungumza mbele ya umati wa watu
waliohudhuria mazishi ya Mbunge wa Chalinze, Saidi Bwanamdogo mwishoni
mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete ambaye alifika katika eneo la makaburi,
alimuuliza Mwenyekiti huyo wa Simba kuhusiana na maandalizi ya mkutano
huo."Ndugu yangu Rage mimi Mwenyekiti mwenzio, lakini sijawahi kuona mkutano wenye ajenda moja ndio kwanza huo wa kwako, yaani wewe kiboko, pamoja na makelele yote lakini umeweza kutuliza hali ya mambo mpaka leo umedumu kuwa mwenyekiti," alisikika Rais Kikwete akisema huku mamia ya waombolezaji wakicheka.
Akizungumzia kauli hiyo ya Rais Kikwete, Rage alisema ili kuwa kiongozi imara ndani ya klabu za Simba na Yanga, inakupasa kuwa na roho ngumu, kwani bila ya kufanya hivyo wanachama watakuwa wakikuchezea kila kukicha.
"Mheshimiwa Rais kuwa kiongozi ndani ya klabu hizi mbili kunahitaji umakini sana, kwani bila ya kufanya hivyo wewe utakuwa ni kiongozi wa kupelekwa kila siku na hatimaye unamaliza muda hakuna ulichokifanya ndani ya uongozi wako," alisema Rage.
SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA UINGEREZA LAKABIDHI VIFAA VYA THAMANI YA TSH.MILIONI 20 KWA MAFUNDI WADOGO
Katibu
tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana, akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vifaa kwa mafundi wadogo wa useremala,ushonaji wa nguo,uhunzi
na ujenzi.Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 20
milioni,vimetolewa na shirika la Tools for self reliance la nchini Wales
Uingereza na zimepitia SIDO mkoa wa Singida.
Katibu
tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana (wa pili kulia) akikabidhi
cherehani kwa mmoja wa kiongozi wa vikundi 17 vilivyonufaika na msaada
wa vifaa vya ufundi vilivyotolewa na shirika la Tools for self reliance
la nchini Wales Uingereza.Wa kwanza kulia ni meneja wa SIDO mkoa wa
Singida, Shoma Kibende.
Katibu
tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana, akiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi wa vikundi 17 vya mafundi wa fani mbalimbali muda mfupi baada
ya kuwakabidhi vifaa vya ufundi vilivyotolewa na shirika la Tools for
self reliance la nchini Wales Uingereza.Wa kwanza kushoto ni mejena wa
SIDO mkoa wa Singida.Shoma Kibende.(Picha na Nathaniel Limu).
Monday, January 20, 2014
WAAOMBA VYUO VYA SIASA KUREJESHWA
Na Lucas Raphael ,Tabora.
Wanaharakati mkoani Tabora
wamemuomba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mh Jakaya
Mrisho Kikwete kufanya utaratibu wa kurudisha vyuo vya siasa hapa nchini ili
wananchi hasa wanaotarajia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa
siasa kufundishwa na kupigwa msasa ili kugombea nafasi hizo wakiwa na
uelewa wa kutosha.
Wakiongea na waandishi wa habari jana
mjini Tabora baadhi ya wanahabari hao walisema kuwa tatizo la kuwa na viongozi
wasiokuwa na maadili limekuwa likichangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea
wasiokuwa na uelewa wa kutosha kujiingiza katika siasa na hatimaye
kuwapotosha wanachi badala ya kuwaambia ukweli halisi wa mbambo yanavyokwenda.
“Siku hizi siyo kama zamani,kijana
anakurupuka kutoka chuo kikuu kwa kuwa ni msomi na wala hajasoma siasa anaenda
anagombea nafasi yeyote ya kisiasa na anachaguliwa ,unategemea huyu ambaye
hajui siasa hata kidogo ataiambia nini jamii kama siyo kuipotosha? Na hiki
dicho chanzo cha kuwapata viongozi wasiokuwa na maadili”alisema mmoja wa
wanaharakati hao.
Katika hatua nyingine wanaharakati hao
wameeleza kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kupinga
kupongezwa kwa Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli
Edward Lowassa kutokana na jitihada mbali mbali anazozifanya kwa nchi yake.
Walisema hata nchi zilizoendelea zina
utamaduni wa kuwapongeza watu au viongozi waliofanya vitu vya kuigwa ila kwa
nchi yetu mtu anapofanya hivyo inaonekana kama kuna nafasi ya kisiasa anayotaka
kuiwania kumbe sivyo.
Bwana ,Elisha Daudi na Deo
Kahumbi walisema kuwa ni vema mtu anapostahili pongezi kupewa na kufafanua kuwa
Bw Edward Lowassa alionyesha uwezo mkubwa kwa kipindi kifupi cha uongozi wake
akiwa kama Waziri mkuu ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa sekondari za kata
ambapo sasa asilimia 80 ya wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi wanajiunga na
sekondari.
Walisema kuwa wakati nchi ilipokumbwa
na ukame Lowassa alisimamia kuhakikisha anachi wake wanapata msaada wa chakula
hivyo kwa hayo na mengine mengi anayoendelea kufanya hana budi kupongezwa na
wanaobeza kupongezwa huko wanaonyesha kutokukomaa kisiasa.
Aidha Bw,Elisha aliongeza kuwa wote
wanaofanya kazi za maendeleo wanapaswa kupongezwa na siyo kupigwa
vita na kuongeza kuwa kipindi cha uchaguzi hakijafika hivyo sasa ni kufanya
shughuli za maendeleo tu na kuacha majungu.
MWISHO…………..
Friday, January 17, 2014
NHIF’ KUJENGA JENGO LA KITEGA UCHUMI TABORA
Na Lucas Raphael,Tabora
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya -NHIF, umedhamiria kujenga jengo la kitega uchumi
mkoani Tabora litakalokuwa na ghorofa sita.
Hayo
yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Rehan Athuman katika
semina ya wadau mbalimbali wa mfuko huo iliyofanyika juzi katika ukumbi wa
Mtemi Isike Mwana Kiyungi mkoani humo.
Alisema
NHIF imekusudia kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma za afya kwa
wanachama wake hapa nchini na katika siku za usoni mfuko huo una mpango wa
kujenga jengo la kisasa katika mkoa wa Tabora litakalokuwa na ghorofa sita ili
kurahisisha utoaji huduma.
Aidha
alisema mfuko huo umedhamiria kuboresha na kupanua wigo wa utoaji huduma za
afya katika mikoa yote hapa nchini ili wanachama wake waweze kujivunia ubora wa
huduma hizo sambamba na kusajili wanachama wapya kwa wingi zaidi.
Ili
kuboresha huduma za mfuko wa afya ya jamii mkoani Tabora na kusogeza huduma
hizo karibu na wananchi NHIF inakusudia pia kujenga jengo la kituo cha
matibabu katika Manispaa hiyo kwa lengo la kupanua wigo wa huduma hizo.
‘Mikoa
mingi hapa nchini ina upungufu wa vituo vya afya, zahanati na hospitali kubwa,
ndio maana tumeona ipo haja ya kujenga kituo hicho cha matibabu mkoani hapa
kama ambavyo tumedhamiria kufanya katika mikoa mingine pia’, alisema.
Aidha
aliuomba uongozi wa serikali ya mkoa huo kushikamana na kuongeza hamasa kwa
wananchi ili waweze kujiunga na kufaidi huduma mbalimbali za kiafya zitolewazo
na mfuko huo.
Mkuu
wa Mkoa huo Fatma Mwassa na Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa hiyo Alfred Luanda
walimhakikishia kuwa Manispaa hiyo iko tayari kushirikiana na mfuko huo
sambamba na kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kitega uchumi na kituo
cha matibabu kama mfuko huo ulivyokusudia.
Luanda
aliwataka viongozi wote katika Manispaa hiyo kubadilika kiutendaji kwa kuongeza
ufanisi katika kazi zao badala ya kuendekeza malumbano yasiyokuwa na tija ili
kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika Manispaa hiyo.
‘Manispaa
yetu haishindwi kusajili idadi kubwa ya wanachama katika mfuko wa afya ya
jamii-CHF, kinachotakiwa ni kubadilika tu kiutendaji na kuanza upya
uhamasishaji wa wananchi’, aliongeza.
Katika
mkutano huo wajumbe walipendekeza kiwango cha mchango wa kujiunga katika huduma
hizo za mfuko wa afya ya jamii kwa mwaka kiwe shilingi 10,000 kwa kichwa,
gharama ambayo itamwezesha mhusika kupata huduma za afya katika kituo chochote
kile mkoani humo kwa kutumia kadi maalumu ya tiba.
Mwisho
|
KIKAO CHA WADAU KWA AJILI YA UANZISHWAJI WA MFUKO AFYA YA JAMII TIKA MANISPAA YA TABORA
Baadhi ya Wadau wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo. |
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw.Yahaya Nawanda na Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu ambao walihudhuria katika mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya Jamii mjini Tabora. |
Diwani wa kata ya Malolo manispaa ya Tabora Bi.Zinduna Kambangwa ambaye alihudhuria mkutano huo wa wadau wa mfuko wa Afya ya Jamii. |
Diwani wa kata ya Kitete Bw.Daniel Mhina alihudhuria katika mkutano huo akisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ambazo zilionesha mafanikio makubwa ya mfuko wa Afya ya Jamii. |
Maafisa wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya walipiga picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya mkoa wa Tabora na wilaya ya Iramba. |
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA.
MATIBABU KWA KADI
MKUU wa mkoa wa wa Tabora FATUMA MWASSA ameiagiza Halmashauri
ya Manispaa ya Tabora ihakikishe upatikanaji wa huduma bora za afya zinazotolewa katika mpango wa matibabu kwa kadi TIKA
zinazokusudiwa kutolewa kwenye manispaa hiyo.
Pia ametaka huduma za zitolewazo katika vituo vyote vya afya
katika Manispaaya Tabora zinakuwa bora ikiwa ni pamoja na kuwepo Lugha nzuri
kwa wanachama mfuko huo sanjali na upatikanaji wa dawa kwa wingi na vifaa tiba.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikako cha
wadau wa mfuko wa afya jamii mijini TIKA, katika manispaa ya Tabora
kilichafanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora.
Akizungumza katika kikao hicho, mama Mwasa amesema fedha za
michango ya wanachama ni lazima zitumike kununulia dawa na kuitaka Halmashauri
hiyo ihakikishe kuwa mongozo wa matumizi ya fedha hizo unafuatwa kikamilifu kwa
lengo la kutimiza azima yake.
Amesema kuwa ofizi ya mkuu wa mkoa na ofisi ya katibu Tawala
wa mkoa haitakubali wala hatakuwa tayari kupokea sababu yoyote ya wananchi
kutopata huduma ya afya baada ya kuwa wamechangia huduma hiyo.
Mama Mwassa ameitaka Halmashauri hiyo kushirikiana na mfuko wa
taifa wa bima ya afya kuendesha kampeni ya kuhamasisha wananchi ili kujiunga na
mpango wa tika kwa kadi kwa lengo la kurahisisha upatikananji wa huduma za afya
kwa gharama nafuu.
Mapema mkurugenzi wa CHF na kaimu mkurugenzi wa mfuko wa taifa
ya bima ya afya ,REHANI ATHUMANI amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa
mpango huo ni kumrahisishia mwananchi kupata
huduma ya afya kwa bei nafuu.
MWISHO
Thursday, January 16, 2014
MADIWANI SINGIDA WAAGIZWA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MAAFISA MALIASILI
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya
upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma
wilaya ya Singida. Wakwanza kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Protace Magayane,anayefuatia katibu
tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju
Msambya. tatu kutoka kushoto (waliokaa). Jumla ya miti 2,200 ilipandwa
kwenye siku ya uzinduzi upandaji Miti kwa mkoa wa Singida,unaotarajia
kupanda miti ya aina mbalimbali zaidi ya milioni moja.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akishiriki kupanda miti kwenye siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Ikungi.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane,
akishiriki kupanda miti kwenye siku ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa
uliofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya
Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
.wengi wa maafisa hao wanajihusisha na biashara haramu ya mkaa
Na Nathaniel Limu, Ikungi
MADIWANI
wa Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa ya Singida wameagizwa kuwachukulia
hatua kali za kisheria maafisa maliasili watakaobainika wanasaidia
kuendeleza biashara ya mkaa.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone wakati
akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji Miti kimkoa uliofanyika kwenye
kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Ikungi.
Amesema
pamoja na kupigwa marufuku kwa biashara ya mkaa mkoani humu,biashara
hiyo inayotishia mkoa kugeuka kuwa jangwa,bado imeendelea kushamiri hasa
katika wilaya ya Ikungi na Manyoni.
“Hapa
wilaya ya Ikungi katika vijiji vya Mkiwa na Issuna,biashara ya mkaa
inafanyika kwa kiwango cha kutisha na maafisa misitu wa ngazi mbalimbali
wakiangalia bila kuchukua hatua zo zote za kukomesha biashara
hii”,amesema Dk.Kone.
Mkuu
huyo wa mkoa,amesema ili mapambano dhidi ya biashara ya mkaa yaweze
kufanikiwa ni kuwaondoa maafisa maliasili wanaosaidia kuendelea biashara
hiyo haramu na kuweka wengine wenye moyo wa kukomesha biashara ya mkaa.
Katika
hatua nyingine,Dk.Kone amewataka wanakikundi cha nyumba ya nyuki cha
kijiji cha Nkuninkana,kuhakikisha kinapanda miti mingi ya maua kwa ajili
ya chakula cha nyuki waliopo kwenye shamba lao.
“Hakikisheni
bwawa lenu la maji linakuwa na maji ya kutosha kipindi chote.Nyuki bila
kuwepo kwa maji na maua ya kutosha ni lazima watahama”,alitahadharisha.
Kikundi
hicho kinachojishughulisha na ufugaji nyuki wakubwa (mizinga 123) na
wadogo mizinga mitatu,kimezawadiwa shilingi laki tatu na mkuu wa mkoa wa
Singida shilingi laki tatu na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju
Msambya,amekichangia shilingi laki mbili.
POLISI WAUA RAIA ULYANKULU TABORA KWA RISASI,WAJERUHI MMOJA
Askari Polisi wa
kituo kidogo cha Tarafa ya Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora wamemuua kwa
kumpiga risasi begani kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la John Joseph(28) kwa tuhuma
za kuleta vurugu na kutaka kuchoma
moto Kituo hicho cha
Polisi,wakiwashurutisha askari hao kumwachia
mtuhumiwa mmoja wa wizi
wa ng’ombe ili waweze kumwadhibu wenyewe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Peter Ouma
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amelieza mtanzania kuwa marehemu
John Joseph juzi majira ya saa tano asubuhi akiwa na wananchi wengine
walimkamata kijana mmoja Shija Matenga(23)kwa
tuhuma za kuiba ng’ombe watano huko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambaye
aliwaswaga hadi eneo la Ulyankulu wilayani Kaliuawa ambako alikamatwa na kuanza
kupigwa.
Ouma alifafanua kuwa
wakati kundi la wananchi hao ambao
miongoni mwao akiwemo
marehemu Joseph wakiendelea kumshambulia mtuhumiwa huyo wa wizi wa mifugo Shija
Matenga,askari Polisi wa
kituo hicho cha
King’wangoko kilichopo tarafa ya
Ulyankulu chini ya uongozi wa mkuu wa
Kituo hicho namba E.1295 D/SGT
KIMOLA walipata taarifa hiyo na
hivyo askari wawili waliagizwa kufika
eneo la tukio kujaribu kuwazuia wananchi
hao ambao tayari walikwisha mfunga kamba mtuhumiwa huku wakikusanya majani kwa
lengo la kutaka kumchoma moto.
Kwa mujibu wa Kamanda Ouma baada ya askari hao
kufanikiwa kumuokoa mtuhumiwa
walimfikisha kituoni wakati kundi
la wananchi hao likiwafuatilia
kwa nyuma wakiwa wanawarushia mawe,chupa na fimbo askari
Polisi hao ambao nao wakalazimika kujikinga kwa kufyatua risasi iliyompata John
Joseph begani na hatimaye kufariki dunia hatua chache
kutoka Kituoni hapo.
Katika sakata hilo lililodumu kwa muda mfupi Malembeka Matemele(22)ambaye ni mkazi wa
Ulyankulu alipigwa risasi paja la mguu wa kulia huku kamanda Ouma akimtaja kuwa
ni mmoja kati ya vinara wa vurugu hizo zilizosababisha mauaji ya mtu mmoja.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa tarafa ya Ulyankulu ambao
hawakutaka majina yao yatajwe hadharani wamelitupia lawama Jeshi la Polisi kwa
kufanya mauaji hayo ya raia asiyekuwa na hatia.
Wamesema wakati wa purukushani hizo zikiendelea
marehemu John alipigwa risasi akiwa anatokea nyumbani kwake hatua ambayo
wamelitafsiri tukio hilo kuwa ni la kinyama na huku wakiziomba taasisi
zinazotetea haki za binadamu kufuatilia na kuchunguza ukweli wa tukio hilo la
maonezi.
DC IRAMBA AWAFUNDA MADIWANI WA MANISPAA YA TABORA KUHUSU MFUKO WA AFYA YA JAMII
Wadau waliendelea kuwa makini kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa NHIF/CHF. |
WAKULIMA WA TUMBAKU KISANGA WATENGA MIL 5.1 KUWEKA UMEME KIJIJINI
Viongozi wa Chama cha Msingi cha wakulima wa Tumbaku Kisanga, kutoka kushoto ni mwenyekiti wa chama hicho Rashid Mazinge akifuatiwa na diwani wa kata hiyo Abdallah Msumeno (Picha na Alan Mtana) |
CHAMA Cha Msingi cha Wakulima wa Tumbaku katika kata ya Kisanga
wilayani Sikonge mkoani Tabora kimetenga sh 5,100,000 za mauzo ya
tumbaku kwa msimu wa 2013/2014 kwa ajili ya kutunisha mfuko maalumu wa
kuweka umeme katika kata hiyo yenye vijiji 3.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Rashid Mazinge, katika
taarifa yake kwa waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho wiki
iliyopita.
Alisema chama hicho chenye jumla ya wanachama 700 kimekusudia kuweka
umeme katika makao makuu ya kata hiyo yaliyoko katika kijiji cha
Kisanga na vijiji vyake na kwa kuanzia wameanzisha mfuko maalumu wa
umeme kwa ajili ya kutimiza lengo hilo.
Aidha alisema wametenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya maandalizi
ya awali ambapo wataanza kwa kununua vifaa mbalimbali vya umeme
ikiwemo vifaa vya komputa na printa vitakavyosaidia kurahisisha
shughuli mbalimbali za ki-ofisi katika ofisi ya chama hicho, tayari
komputa kadhaa zimeshanunuliwa.
‘Ndugu waandishi wa habari, tumekusudia kuweka umeme katika kijiji
chetu ndio maana tumeanza kukusanya fedha na kuzitunza kama
wanakikundi, mda si mrefu tutaenda wilayani kufuatilia taratibu
zingine, tunaomba na ninyi mtusaidie huko wilayani ili tufanikiwe
haraka’, alisema.
Alibainisha kuwa chama kimefikia hatua hiyo baada ya kupata mafanikio
makubwa katika msimu wa 2012/2013 na 2013/2014 hali iliyowafanya
wanachama wake kwa kauli moja kuridhia haja ya kuanzishwa mfuko huo
ili kujiletea maendeleo katika kata hiyo yenye vijiji 3 (Utyatya,
Mwamayunga na Kisanga).
Katika msimu wa 2012/2013 chama hicho kilizalisha jumla ya kilo
940,049 za tumbaku zenye thamani ya Dola za kimarekani 2,538,132 (sawa
na sh bil 4.1) na mapato ya ushuru yalikuwa dola za kimarekani 65,000
(sawa na sh mil 103.4), kwa mapato hayo waliweza kulipa deni la
pembejeo la dola 692,000.(sawa na sh bil 1.1) kutoka benki ya NMB na
kubakiwa na fedha ya kutosha.
Aidha katika msimu wa 2013/2014 walilenga kuzalisha jumla ya kilo
1,400,000 zenye thamani ya Dola 3,920,000 sawa na sh bilioni 6.3 na
mapato ya ushuru walilenga kukusanya dola 98,000 sawa na sh mil 156.8
hali ambayo itawawezesha kulipa deni la pembejeo dola 968,000 sawa na
sh bil 1.5 toka NMB.
Alitaja mafanikio ya chama hicho kuwa ni kuanzishwa mfuko wa ujenzi wa
ghala la kuhifadhia tumbaku ambao umetengewa kiasi cha Dola 31,000 (sh
mil 49.3), ujenzi wa ofisi ya kata ambapo chama hicho kimechangia sh
mil 3, kuanzisha mfuko wa umeme, kuanzisha KISANGA SACCOS LTD ambayo
mpaka sasa ina jumla ya Dola 21,000 (sawa na sh mil 33,495,000).
Alisema chama hicho kimedhamiria kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo
kupitia vikao mbalimbali vya wanachama wake ambapo kimetenga sh
milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa gari aina ya FUSO ili kurahisisha
huduma mbalimbali za wakulima kijijini hapo, pia kimekusudia kukusanya
Dola 84,000 (sh mil 134,000,000) ili kuongeza nguvu ya SACCOS yao.
Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto kadhaa zinazowakabili ikiwemo
mikopo na bei kubwa za pembejeo, ucheleweshaji na upatikanaji wa
pembejeo hizo, kutokuwa na umeme, ubovu wa barabara zinazounganisha
vijiji hivyo, ukosefu wa maji safi na salama, ukosefu wa nyumba ya
mganga wa zahanati na kituo cha polisi.
Diwani wa kata hiyo Abdallah Msumeno mbali na kupongeza hatua ya chama
hicho kutenga sh mil 2 kwa ajili ya kununua viti 100 vya plastic na
kutenga sh 576,000 za michango ya wanachama katika mfuko wa NSSF pia
ametoa wito kwa wakulima hao kufuata kalenda ya msimu wa kilimo ili
kupata mafanikio zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)