Monday, January 6, 2014

"CHADEMA CHAMA CHA KIFAMILIA"-MUNDE

Mbunge wa vitmaalum mkoani Tabora Bi.Munde Tambwe akijibu maswali ya wananchi katika mkutano wa hadhara ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana tangu achaguliwe kushika wadhifa huo.
"Msikubali hoja zinazotolewa na wapinzani eti serikali ya CCM haijafanya lolote hilo si kweli,wao wasiwadanganye kwamba wataleta mabadiliko si kweli,wanapiga picha na kupeleka kwa wafadhili wanapata pesa kwa manufaa yao binafsi,ni matajiri wakubwa hao waupuuzeni,kwanza Chama chao ni cha kifamilia"alisema Mheshimiwa Munde wakati akiwa jukwaani katika mkutano uliofanyika kata ya Gongoni manispaa ya Tabora.    
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Moshi Abrahamu akikabidhi msaada wa shilingi laki tano kama sehemu ya kukichangia kikundi cha Wajasiliamali cha Wanawake wa kata ya Gongoni.
Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Aden Rage naye alipata fursa ya kuongea na wananchi na baadae kuulizwa maswali.
Viongozi waliohudhuria katika mkutano huo wa wahadhara.
Ufunguzi wa tawi wa Wanawake wa CCM tawi la Gongoni
Mbunge wa vitimaalum mkoani Tabora Bi.Munde Tambwe akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa tawi la UWT Kata ya Gongoni mjini Tabora.
Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara.
Mjumbe wa halmashauri ya CCM kutoka mkoani Tabora Bw.John Mchele akizungumza na wananchi katika mkutano huo ambapo aliwataka Wananchi kuendelea kukiunga mkono CCM ili kiweze kutekeleza adhma yake ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.



No comments:

Post a Comment