DC IRAMBA AWAFUNDA MADIWANI WA MANISPAA YA TABORA KUHUSU MFUKO WA AFYA YA JAMII
Mkuu
wa wilaya ya Iramba Bw.Yahaya Nawanda akizungumza katika mkutano wa
wadau kuhusu uanzishwaji wa mfuko wa Afya ya Jamii Manispaa ya
Tabora,mkuu huyo ameshiriki katika mkutano huo kwa lengo la kutoa
maelezo namna Wilaya yake ilivyofanikiwa kuihamasisha Jamii kuchangia
mfuko huo unaotoa huduma ya Afya kwa kutumia Kadi katika
hospitali,zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na halmashauri.
Baadhi
ya wadau wakiwemo Watendaji wa mitaa,Kata na vijiji wakimsikiliza kwa
makini mkuu wa wilaya ya Iramba ambapo pia aliwataka Madiwani kusaidiana
na Watendaji hao kuhamasisha Jamii iweze kujiunga na Mpango huo wa Tiba
kwa Kadi(TIKA)
Mkuu
wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya,Mwakilishi wa mkurugenzi wa
NHIF Taifa Bw.Athuman Rehani na mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki
Kingu wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Iramba katika mkutano
huo wa wadau.
''Madiwani
wasaidieni wananchi kujenga uchumi wao ili iwe rahisi kuwahamasisha
kuchangia mfuko wa Afya ya Jamii hatua ambayo pia itawasaidia kuwajengea
mazingira mazuri ya kurejea kwenye nafasi zenu kwenye uchaguzi mkuu
wa 2015"Alisema Bw.Nawanda.
Wadau waliendelea kuwa makini kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa NHIF/CHF.
No comments:
Post a Comment