Thursday, January 16, 2014

MADIWANI SINGIDA WAAGIZWA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MAAFISA MALIASILI


Picture 505
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Singida. Wakwanza kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Protace Magayane,anayefuatia katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya. tatu kutoka kushoto (waliokaa). Jumla ya miti 2,200 ilipandwa kwenye siku ya uzinduzi upandaji Miti kwa mkoa wa Singida,unaotarajia kupanda miti ya aina mbalimbali zaidi ya milioni moja.
Picture 524
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akishiriki kupanda miti kwenye siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Ikungi.
Picture 529
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane, akishiriki kupanda miti kwenye siku ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa uliofanyika katika kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Singida.(Picha na  Nathaniel Limu).
.wengi wa maafisa hao wanajihusisha na biashara haramu ya mkaa
Na Nathaniel Limu, Ikungi
 
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa ya Singida wameagizwa kuwachukulia hatua kali za kisheria maafisa maliasili watakaobainika wanasaidia kuendeleza biashara ya mkaa.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji Miti kimkoa uliofanyika kwenye kijiji cha Nkuninkana kata ya Puma wilaya ya Ikungi.

Amesema pamoja na kupigwa marufuku kwa biashara ya mkaa mkoani humu,biashara hiyo inayotishia mkoa kugeuka kuwa jangwa,bado imeendelea kushamiri hasa katika wilaya ya Ikungi na Manyoni.

“Hapa wilaya ya Ikungi katika vijiji vya Mkiwa na Issuna,biashara ya mkaa inafanyika kwa kiwango cha kutisha na maafisa misitu wa ngazi mbalimbali wakiangalia bila kuchukua hatua zo zote za kukomesha biashara hii”,amesema Dk.Kone.

Mkuu huyo wa mkoa,amesema ili mapambano dhidi ya biashara ya mkaa yaweze kufanikiwa ni kuwaondoa maafisa maliasili wanaosaidia kuendelea biashara hiyo haramu na kuweka wengine wenye moyo wa kukomesha biashara ya mkaa.

Katika hatua nyingine,Dk.Kone amewataka wanakikundi cha nyumba ya nyuki cha kijiji cha Nkuninkana,kuhakikisha kinapanda miti mingi ya maua kwa ajili ya chakula cha nyuki waliopo kwenye shamba lao.

“Hakikisheni bwawa lenu la maji linakuwa na maji ya kutosha kipindi chote.Nyuki bila kuwepo kwa maji na maua ya kutosha ni lazima watahama”,alitahadharisha.

Kikundi hicho kinachojishughulisha na ufugaji nyuki wakubwa (mizinga 123) na wadogo mizinga mitatu,kimezawadiwa  shilingi laki tatu na mkuu wa mkoa wa Singida shilingi laki tatu na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya,amekichangia shilingi laki mbili.

No comments:

Post a Comment