Na Lucas Raphael ,Tabora.
Wanaharakati mkoani Tabora
wamemuomba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mh Jakaya
Mrisho Kikwete kufanya utaratibu wa kurudisha vyuo vya siasa hapa nchini ili
wananchi hasa wanaotarajia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa
siasa kufundishwa na kupigwa msasa ili kugombea nafasi hizo wakiwa na
uelewa wa kutosha.
Wakiongea na waandishi wa habari jana
mjini Tabora baadhi ya wanahabari hao walisema kuwa tatizo la kuwa na viongozi
wasiokuwa na maadili limekuwa likichangiwa kwa kiasi kikubwa na wagombea
wasiokuwa na uelewa wa kutosha kujiingiza katika siasa na hatimaye
kuwapotosha wanachi badala ya kuwaambia ukweli halisi wa mbambo yanavyokwenda.
“Siku hizi siyo kama zamani,kijana
anakurupuka kutoka chuo kikuu kwa kuwa ni msomi na wala hajasoma siasa anaenda
anagombea nafasi yeyote ya kisiasa na anachaguliwa ,unategemea huyu ambaye
hajui siasa hata kidogo ataiambia nini jamii kama siyo kuipotosha? Na hiki
dicho chanzo cha kuwapata viongozi wasiokuwa na maadili”alisema mmoja wa
wanaharakati hao.
Katika hatua nyingine wanaharakati hao
wameeleza kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wanasiasa kupinga
kupongezwa kwa Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli
Edward Lowassa kutokana na jitihada mbali mbali anazozifanya kwa nchi yake.
Walisema hata nchi zilizoendelea zina
utamaduni wa kuwapongeza watu au viongozi waliofanya vitu vya kuigwa ila kwa
nchi yetu mtu anapofanya hivyo inaonekana kama kuna nafasi ya kisiasa anayotaka
kuiwania kumbe sivyo.
Bwana ,Elisha Daudi na Deo
Kahumbi walisema kuwa ni vema mtu anapostahili pongezi kupewa na kufafanua kuwa
Bw Edward Lowassa alionyesha uwezo mkubwa kwa kipindi kifupi cha uongozi wake
akiwa kama Waziri mkuu ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa sekondari za kata
ambapo sasa asilimia 80 ya wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi wanajiunga na
sekondari.
Walisema kuwa wakati nchi ilipokumbwa
na ukame Lowassa alisimamia kuhakikisha anachi wake wanapata msaada wa chakula
hivyo kwa hayo na mengine mengi anayoendelea kufanya hana budi kupongezwa na
wanaobeza kupongezwa huko wanaonyesha kutokukomaa kisiasa.
Aidha Bw,Elisha aliongeza kuwa wote
wanaofanya kazi za maendeleo wanapaswa kupongezwa na siyo kupigwa
vita na kuongeza kuwa kipindi cha uchaguzi hakijafika hivyo sasa ni kufanya
shughuli za maendeleo tu na kuacha majungu.
MWISHO…………..
No comments:
Post a Comment