Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji.
.Madiwani waazimia Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji asimamie maombi
Na Nathaniel Limu, Singida
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Singida inatarajia kuwasilisha serikalini maombi maalum
ya kuomba jumla ya shilingi 3.5 bilioni kwa ajili ya kugharamia maeneo
manne ambayo ni ya kipaumbele katika mwaka wake wa fedha wa 2014/2015.
Hayo
yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Singida,Deus Lusiga wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka
ujao wa fedha mbele ya kikao maalum ya baraza la madiwani kilichofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.
Amesema
Manispaa ya Singida imefikia uamuzi huo kutokana na ufinyu wa mapato na
uwepo wa changamoto ya kujitosheleza katika mahitaji yake.
Lusiga
alitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la
Manispaa linalotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi 2.7 bilioni.
Kaimu
Mkurugenzi huyo alitaja vipaumbele vingine kuwa ni ununuzi wa gari na
vifaa vya kuzolea taka ngumu na maji ambayo itagharimu 300
milioni,ujenzi wa madaraja,milioni 200 na ukamilishaji wa nyumba za
walimu na madarasa katika shule za msingi ambapo zitatumika shilingi 300
milioni.
Kikao
hicho kilichokuwa chini ya Mstahiki Meya,Sheikh Salum Mahami kwa kauli
moja kimeazimia kwamba Mbunge wa Jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam
Dewji asimamie maombi serikali ili matarajio yaweze kufikiwa.
Awali
akifungua kikao hicho,Mstahiki Meya Sheikh Mahami alitumia fursa hiyo
kuviomba vyombo vya habari kuitangaza vema na kwa usahihi bajeti hiyoili
pamoja na mambo mengine jamii iweze kufahamu uwezo wa Manispaa yao
katika kuwahudumia na kuwaletea maendeleo endelevu.
“Katika
vikao hivi vya bajeti,vyombo vya habari ni muhimu mno kuwepo vitasaidia
sana wananchi kujua bajeti ya mwaka husika ya Manispaa yetu na
inatarajia kutekeleza miradi ipi ya maendeleo katika mwaka wa fedha
husika”,alifafanua Sheikh Mahami.
No comments:
Post a Comment