Baadhi ya Wadau wakiwa katika ukumbi wa mkutano huo. |
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw.Yahaya Nawanda na Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu ambao walihudhuria katika mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya Jamii mjini Tabora. |
Diwani wa kata ya Malolo manispaa ya Tabora Bi.Zinduna Kambangwa ambaye alihudhuria mkutano huo wa wadau wa mfuko wa Afya ya Jamii. |
Diwani wa kata ya Kitete Bw.Daniel Mhina alihudhuria katika mkutano huo akisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa ambazo zilionesha mafanikio makubwa ya mfuko wa Afya ya Jamii. |
Maafisa wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya walipiga picha ya pamoja na viongozi wa Serikali ya mkoa wa Tabora na wilaya ya Iramba. |
NA LUCAS RAPHAEL,TABORA.
MATIBABU KWA KADI
MKUU wa mkoa wa wa Tabora FATUMA MWASSA ameiagiza Halmashauri
ya Manispaa ya Tabora ihakikishe upatikanaji wa huduma bora za afya zinazotolewa katika mpango wa matibabu kwa kadi TIKA
zinazokusudiwa kutolewa kwenye manispaa hiyo.
Pia ametaka huduma za zitolewazo katika vituo vyote vya afya
katika Manispaaya Tabora zinakuwa bora ikiwa ni pamoja na kuwepo Lugha nzuri
kwa wanachama mfuko huo sanjali na upatikanaji wa dawa kwa wingi na vifaa tiba.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikako cha
wadau wa mfuko wa afya jamii mijini TIKA, katika manispaa ya Tabora
kilichafanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora.
Akizungumza katika kikao hicho, mama Mwasa amesema fedha za
michango ya wanachama ni lazima zitumike kununulia dawa na kuitaka Halmashauri
hiyo ihakikishe kuwa mongozo wa matumizi ya fedha hizo unafuatwa kikamilifu kwa
lengo la kutimiza azima yake.
Amesema kuwa ofizi ya mkuu wa mkoa na ofisi ya katibu Tawala
wa mkoa haitakubali wala hatakuwa tayari kupokea sababu yoyote ya wananchi
kutopata huduma ya afya baada ya kuwa wamechangia huduma hiyo.
Mama Mwassa ameitaka Halmashauri hiyo kushirikiana na mfuko wa
taifa wa bima ya afya kuendesha kampeni ya kuhamasisha wananchi ili kujiunga na
mpango wa tika kwa kadi kwa lengo la kurahisisha upatikananji wa huduma za afya
kwa gharama nafuu.
Mapema mkurugenzi wa CHF na kaimu mkurugenzi wa mfuko wa taifa
ya bima ya afya ,REHANI ATHUMANI amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa
mpango huo ni kumrahisishia mwananchi kupata
huduma ya afya kwa bei nafuu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment