Monday, January 6, 2014

"UVCCM TABORA MJINI WAKAMILISHA ZIARA YA BUTIAMA NA KENYA,WAREJEA NYUMBANI KWA KISHINDO"


Baadhi ya vijana wa UVCCM muda mfupi mara baada ya kuwasili Tabora ambapo walipokelewa kwa Shangwe kubwa wakitokea mkoani Mara ziara ya kichama ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwawezesha vijana kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo.

Mlezi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Emmanuel Mwakasaka akizungumza na vijana hao baada ya kuwasili Orion Tabora Hotel baada ya kukamilisha ziara yao mkoa wa Mara ambapo walitembelea Kaburi la Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere,pia wakatembelea maeneo mbalimbali nchini Kenya wakijifunza masuala ya Maendeleo.
Kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Tabora Bw.Lucas Masanja akielezea mafanikio makubwa ya ziara yao iliyochukua muda wa siku tano ambapo vijana hawa walipata fursa ya kuzungumza na Mmoja kati ya wabunge mashuhuri Mh.Nimrod Mkono ambaye aliwatembeza na kujionea maendeleo makubwa katika nyanja za elimu,Afya na Kilimo ambayo yametekelezwa na mbunge huyo na tena kwa fedha zake binafsi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Sekondari,Chuo kikuu,Zahanati  pamoja na mashamba makubwa ya mfano yanayotumiwa na Serikali mkoani Mara.
''Kwakweli Wabunge wa wenzetu huko tulikotoka wanatekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo na huo ni mfano wa kuigwa kwa wale wote wanaopata dhamana ya kuongoza"alisema Masanja
''Kwa yale tuliyoyaona na kujifunza tumehamasika nasi tutayafanya hapa ili iwe changamoto kwa vijana wenzetu kuiga mfano huo wa maendeleo"
"Kwa uwezo wa Mwenyezimungu tutahakikisha ziara itakayofuata tutawezesha vijana wengi zaidi washiriki ziara hiyo maana itasaidia kuwajenga kifikra na pia kujenga mahusiano mazuri na vijana wengine wa UVCCM ambapo itazidisha kuwafanya kuwa wazalendo kwa nchi yao"alisema Mwakasaka
Ukafika wakati baada ya kupata chakula cha jioni hapo Orion Tabora Hotel kilichoambatana na vinywaji na kuwafanya vijana hawa kuondokana na hali ya Uchovu,sasa walianza kulisakata dansi maalumu kwa ajili yao lililoporomoshwa na One Temi Band ambapo dereva wa CCM wilaya ya Tabora mjini  Bw.Kaswalala  alilazimika kujifunza kucheza KIDUKU kwa muda huo lakini alishindwa kutokana na Uchangamfu aliokuwanao.
Uchangamfu ulizidi na mambo yakawa kama hivi......






No comments:

Post a Comment