NA LUCAS RAPHAELNZEGA
Hayo yalisemwa na
Naibu waziri wa Nishati
na Madini Steven Masele kuwa serikali imelidhia maombi
ya wachimbaji ambao wameibua mgodi mdogo pembezoni mwa mgodi mkubwa wa dhahabu
wa Resolute Gorden Pride na kuanza kuendesha shuguli hizo bila kufuata taratibu
na sheria za madini.
Kauli hiyo imetolewa
baada ya Serikali ya wilaya na ofisi za madini Tabora na shinyanga kusitisha
shuguli za uchimbaji wa dhahabu katika mgodi huo mdogo wa mwanshina hali
iliyopelekea mgogoro baina ya wachimbaji na serikali.
Naibu huyo mwenye
dhamana alisema kuwa serikali itahakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na
rasilimali za Taifa kutokana na wao kuzilinda kwa muda mrefu hivyo wana wajibu
wa kupatiwa kipaumbele katika kupewa maeneo kwa kufuata sheria na taratibu za
madini.
Alisema kuwa serikali
itahakikisha wawekezaji hao wanazungumza na kufikia muafaka ili wapinishe
reseni yao ya umiliki wa eneo hilo ili wachimbaji wadogo waweze kupatiwa resen
ndogo itakayo wapatia fursa ya uchimbaji wa kiharali.
Aliwataka viongozi wa
serikali,chama pamoja na viongozi wa wachimbaji kushirikiana kwa haraka
ilizoezi hilo liweze kukamilika ikiwa na kupatiwa reseni pamoja na wachimbaji
waendelee na shuguli za uzalishaji mali.
Naibu waziri Masele
aliwaahidi wananchi na wachimbaji kuwa suala hilo atalifanyia uharaka mkubwa
ili wachimbaji waendelee na kazi ikiwa na kutatua kero hiyo kwa muda mfupi huku
akitumia uzoefu alikuwa nao.
‘’Tutakacho
kifanya tutakaa na wawekezaji hawa na kuwaambia wapindishe umiliki wa
eneo hilo ili wachimbaji wapate fursa ya kufanya kazi ikiwa na kuwapatia reseni
ndogo ya umiliki harali wa eneo hilo’’alisema Naibu waziri Maselle.
Rais wa shilikisho la
wa chimbaji wadogo nchini John Wambura Bina alimuomba Naibu huyo
kulifanyia kazi suala hilo kwa haraka na kuongeza kuwa viongozi wote wa
serikali waungane kuhakikisha zoezi hilo linatimia ili wananchi wanufaike na
rasilimali zilizopo.
Kwaupande wake Mbunge
wa Jimbo la Nzega Dk,Hamis Kigwangalla alimpongeza Naibu waziri huyo kwa
kuwaahidi wachimbaji hao kutatua kero hiyo ikiwa na kuwapatia reseni ndogo ya
umiliki harali wa eneo hilo.
Baadhi ya wachimbaji
wadogo wa eneo hilo Joseph Mbondo,mihambo Seleli,Erasto shila pamoja na
Charles Yota wakizungumza na waandishi wa habari waliitaka serikali
wialayani humo iweze kumuunga mkono waziri huyo katika kuhakikisha kero hiyo
inatekelezwa mara moja na wachimbaji waendelee na kazi zao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment