Wednesday, December 3, 2014

AIR SEYCHELLES YAZINDUA SAFARI ZA NDEGE MAHE - DAR ES SALAAM

 

 Shirika la Ndege la Taifa la Shelisheli, Air Seychelles limeanza kufanya safari zake kati ya mji mkuu wa nchi hiyo, Mahe na Dar es Salaam ambapo  Desemba 2, 2014, ndege yake ya abiria HM 777 ilifanya safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Ujio wa shirika hilo la ndege unafanya mashirika ya ndege yaliyoanzisha safari zake kuja Dar es Salaam kwa siku za hivi karibuni kufikia matatu, Air Seychelles, Flydubai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Rwandair ya Rwanda. Shirika lingine la ndege, Etihad la Abudhabi (UAE) linatarajiwa kuanza safari zake mwaka 2015.
Ndege ya abiria HM 777  Ya Airseychelles baada ya  safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment