Wednesday, December 17, 2014

MKUU WA MKOA HATOA PONGEZI KWA PSI TABORA

 




Mkuu wa mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameipongeza asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Population Sevices International(PSI) kwa kazi nzuri ya kutoa elimu ya ukimwi kwa njia ya sinema na uzazi wa mpango kwa jamii.

Pongezi hizo alizitoa wakati akikangua mabanda siku ya uzinduzi wa kampeni ya nyota ya kijani  na kutolewa na taarifa ya juu asasi hiyo kutoe elimu ya ukimwi na uzazi wa mpango sehemu mbalimbali mkoani hapa.

Mwananzila alisema kwamba jamii inatakiwa kuwa salama na kuyatuza maisha yao kwa kuzingatia uzazi salama kwa kutumia njia sahihi ya uzazi wa mpango kwa lengo la kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na wato wachanga.

Alisema elimu bado inahijatika sana kwa  jamii hasa maeneo ya mijini na vijiji kwani huko ndiko  elimu hajiafika kiasi cha kutoasha hivyo jududi za dhati zinahitajika ili kuwafikia wananchi walio wengi.

Alisema kiwango cha uzazi nchini kimepungua ila bado ipo juu kwani mwaka 1991-1992 kilikuwa watoto 6.3 kwa kila mwanamke na katika mwaka 2010 kilishuka hadi kufikia watoto 5.4, na kwa vijijini  6.1.

Mwananzila alisema katika maeneo ya vijijini kuna kiwango kikubwa cha kuzaliana na elimu haijawafikia walengwa hivyo serikali ina mikakati ya kupeleka elimu pamoja na huduma katika maeneo hayo ili kuwa karibu na kupandisha wastani wa Taifa wa asilimia 60 ifikapo mwaka 2015.

Awali meneja mauzo  wa psi mkoa wa tabora, Gabriel Setumbi alisema kwamba asasi yake tayari imefikia vijiji vipatavyo 89 kwa ajili ya kutoa elimu ya ukimwi kwa njia ya sinema .

Aidha alisema licha ya kutoa elimu ya sinema lakini pia wamekuwa wakisambaza biddha za afya kwa ajili ya  kupambana na mambukizi ya ukimwi uzazi za mpango.

Alisema kwamba asasi hiyo inashirikia na wizara ya afya kuhakikisha itoa huduma sahihi ya uzazi wa mpango kwa kinamama na wanaume katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Tabora.

Mwisho


No comments:

Post a Comment