Wednesday, December 3, 2014

ALIYEWAKOSOA SASHA NA MALIA AJIHUZULU

 

Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House

Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.

Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

No comments:

Post a Comment