Wednesday, December 3, 2014

UWANJA WA NDEGE MPANDA WAASWA KUTUNZA MIUNDOMBINU

 

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo uwanjani hapo.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia). Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango).

Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto). Anayewasikiliza ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah (Katikati).
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelekezo ya uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kutoka kwa Meneja wa uwanja huo, Bw. Seneti Lyatuu (Kushoto).
Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kushoto) akimuonesha kitu Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni wajumbe wa timu hiyo.
Sehemu ya Uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya barabara ya kutua na kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda. PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

Na Saidi Mkabakuli, Mpanda
Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment